Mtoto
Grace Magori mwenye umri wa miaka 12 ambaye yupo 6 grade (darasa la 6)
Columbia, Maryland mchini Marekani anazidi kupaa baada ya siku ya
Jumamosi Novemba 15, 20`14 kuimba kwenye onyesho lililobeba jina la
"Studio Recital" katika uimbaji huo ambo Grace Magori ndio mtoto pekee
aliyeimba nyimbo alizoandika na kuzitengeneza yeye mwenyewe. Watoto
wengine waliokuwepo kwenye onesho hilo ni Jack Zhao aliyeimba wimbo wa
mahadhi ya Kihindi, Cindy Zhao aliyeimba wimbo wa Willie and Tillie-
Swan Lake, Kaitlyn Mummert aliyeimba wimbo wa The Swing- Cossack Ride,
Sara Shapiro wimbo wa Children of Eden. Watoto wengine walikua Caitlyn
Baumgarten na wimbo wa American Honey, Christine Capozzoli wimbo wa O
Mio Babbino Caro na Grace Magori aliyeimba wiimbo wake aliotunga yeye
mwenyewe kwa kuandika na upangaji wa kinanda, wimbo wake unaitwa Badges.
Baba
wa mtoto anaitwa Saria Magori ambaye ndiye aliyeanza kugundua kipaji
cha mwanae mwaka 2012 na baada ya hapo aliendelea kumwendeleza Grace kwa
kumwandikisha kwenye darasa la muziki ambalo Grace anaendelea nalo
mpaka hivi leo na ameonyesha kipaji kinachowashangaza watu wengi kwa
umahiri wake wa kupiga kinanda na kuimba kitu ambacho watoto wenzake
waliofanya nao onesho waliimba tu bila kupiga ala ya muziki yeyyote.
Mwezi
Septemba 2013 alishinda tuzo ya Columbia Talent Show iliyofanyika huko
Columbia Maryland na kuwashangaza wahudhuriaji wa tamasha hilo la vipaji
lililompekelea Grace Magori kuonekana mtu maarufu kwani watu wengi
waliohudhuria tamasha hilo walimuomba mtoto Grace awasainie na yeye bila
kusita alifanya hivyo na wengi walimfananisha na Alicia Keys
mwanamuziki maarufu nchini Marekani anayeimba na kupiga kinanda.
Chini ni Video zilizochukuliwa kwenye onesho lake la jana Baltimore, Maryland.
Wakwanza kulia waliosimama nyuma ni Didi Vava rafiki yake mkubwa Saria akiwa na mama mwenye nyumba wake (koti jeusi) pamoja na watoto wao waliosimama chini ya Didi Vava, Saria na wanae na rafiki yake Grace wakiwa katika picha ya pamoja baada ya kumalizika onesho la muziki la Studio Recital lililofanyika Baltimore, Maryland nchini Marekani.
Grace Magori akiwa na mdogo wake na rafiki yake kitasha.
Chini ni video ya Grace Magori alivyoanza baa ya baba yake kugundua kipaji chake.
0 comments:
Post a Comment