Na Haruni Sanchawa
Wahitimu wa Chuo cha Mlimani School Of Profession walipata msisimko mkubwa baada ya Mkurugenzi Mtendaji wa Global Publishers, Eric Shigongo kutoa hotuba ambayo kila mmoja alijiona kuwa anaweza kujikwamua kimaisha kama wakijibidisha katika maisha yao ya kila siku.
Msisimko huo ulikua pale Shigongo alipotoa simulizi ya riwaya ya ombaomba mmoja aliyekuwa akiomba kila siku kwa kutumia kopo, kumbe kopo lile ni dhahabu yenye thamani ya mabilioni ya fedha kwenya mahafali ya pili katika chuo hicho.
Mmoja wa wahitumu ngazi ya diploma katika fani ya Habari na Mawasiliani ya Umma, Neema Kisimbo alimpongeza Shigongo kuwa ni kati ya Watanzania wachache waliopewa thawabu na Mungu hata kama akifa leo atakuwa na la kusema kuhusu alivyoweza kuisaidi jamii.
“Baba huyu ana kipaji lakini mbali na kipaji chake pia kujituma kwake kumefanya awe na mafanikio makubwa maana maisha ni malengo, si kweli kwamba ameenda kwa waganga,” alisema mhitimu huyo.
Katika mahafali hayo, Shigongo aliwatunuku vyetu wahitimu 119 katika Chuo cha Mlimani School of Profession Studies katika mahali yaliyofanyika katika chuo hicho hapo jana Mbezi Kwa Msugur jijini Dar es Salaam.
Wahitumu hao walifunzu katika kozi tofauti ndani ya chuo hicho ambapo kuna baadhi ya walipata ngazi ya cheti na wengine katika ngazi ya diploma ambapo wote hao walitunukiwa vyeti hivyo na mkurugenzi wa Global Publishars ambaye alikuwa mgeni rasimi katika mahafali hayo.
Mkurugenzi huyo alitoa vyeti kwa wahitimu 19 katika ngazi ya cheti kwa fani ya Manunuzi na Ugavi, Fani ya Habari na Mawasiliano ya Uma wahitimu ngazi ya cheti walikuwa 20, Rasilimali Watu wahitimu 18, ngazi ya cheti wahitimu Uhasibu walikuwa 17 , Uongozi na Biashara ngazi ya cheti sita, Mauzo na Masoko ngazi ya cheti 3, Rasilimali Watu ngazi ya diploma sita , Uongozi wa Biashara diploma 10, Uandishi wa habari na Mawasiliano ya Umma ngazi ya diploma10.
0 comments:
Post a Comment