Monday, November 17, 2014




HABARI


Ripota Elisa Shunda kutoka Dar es salaam ameziwasilisha hizi picha za wakazi wa kata ya Ubungo wakiwa katika msururu wakisubiri kupatiwa vitambulisho vyao vya uraia ambavyo vimekuwa ngumu kuvipata kutokana na mpangilio unaolalamikiwa kuwa mbovu wa mamlaka ya vitambulisho (NIDA).
Baadhi ya wananchi waliofika katika kituo hicho na vingine wamekuwa wakilalamika kutokuona majina yao katika picha na majina yanayobandikwa katika ukuta wa ofisi za mitaa na kata.



Wengine wanasema wafanyakazi wa Mamlaka ya vitambulisho vya taifa (NIDA) wamekuwa wakiwasaidia watu wengine kuwapatia vitambulisho kinyume na utaratibu jambo ambalo huwa linaleta msongamano mkubwa sana na kuwafanya wafanyakazi hao wasifanye kazi zao kwa ufanisi.


Baadhi ya wananchi waliofika katika kituo hicho wakijaribu kuangalia majina yao kama yapo au hayapo ambapo katika kituo kingine baadhi yao walisemahawakuona majina yao japokuwa walijiandikisha katika kituo hicho.


Wananchi wakihangaika kuingia ndani kupatiwa vitambulisho vyao baada ya kuona msafara hauendi na kuna watu wanaingia ndani bila utaratibu maaalumu


Afisa wa mamlaka ya vitambulisho vya taifa (NIDA) akiita majina kwa pembeni ili kurahisisha watu waondoke mapema ila bado wananchi wamelalamikia utaratibu mbovu wa ugawaji wa vitambulisho.

0 comments:

Post a Comment