Monday, November 3, 2014

 Mara Baada ya Ibada katika Kanisa la Azania Front wakati wa kuadhimisha miaka 85 ya kuzaliwa ya aliyekuwa Mkuu
wa Jeshi la Polisi nchini (IGP) Philemoni Mgaya
WAZIRI Mkuu
Mstaafu Cleopa Msuya amewaomba watanzania
kuwa na tabia ya utii wa sheria, uaminifu na uadilifu katika nafasi zao
wanazozitumukia katika Taifa la Tanzania.
Msuya
aliyasema hayo katika sherehe ye kuadhimisha miaka 85 ya kuzaliwa ya aliyekuwa Mkuu
wa Jeshi la Polisi nchini (IGP) Philemoni Mgaya iliyofanyika katika Hotel ya
Protea , Court Yard jijini Dar es Salaam.
Waziri Mkuu
Mstaafu alieleza kuwa tabia aliyoionyesha Mgaya wakati wa utumishi wake
serikalini inapaswa kuigwa na watanzania wote.
“Huyu ndiye
Mtanzania halisi aliyelelewa vizuri kuitumikia nchi yake. Hana makuu, ni mkweli
na mwadilifu. Akiahidi kufanya jambo fulani analitekeleza bila kuchelewa.
Tunahitaji uwajibikaji wa namna hii,” Msuya alisisitiza.
Alisema kuwa
Mgaya alikuwa kiongozi hodari ambaye alisimamia vyema kiapo na kazi zake na
kipindi chake cha uongozi  alikuwa akitoa
amri zinatekelezwa mara moja.
Naye Mshauri
wa kimataifa wa Kujitegemea wa Kampuni ya Mabibo Beer Wines and Spirits Limited
James Rugemalira alitoa wito kwa watanzania kuendele kuunga mkono  jitihada za kuendeleza maeneo mbalimbali ya
kiuchumi ikiwemo viwanda.
Aliwasihi wadau
kutoa ushirikiano kwa  kampuni yake inayosambaza
bia aina ya Windhoek Larger na Windhoek Draught ambayo inadhamira ya kujenga
kiwanda cha kuzalisha bia hizo hapa nchini.
                                       
“Tunatafuta
maeneo Kilimanjaro, Tanga na Bukoba ili tuweze kujenga kiwanda hapa nchini.
Tumedhamilia kufanya hivyo na tutafanya,” Rugemalira alisisitiza.
Naye Mkurugenzi
Mtendaji wa kampuni hiyo Benedicta Rugemalira aliwashukuru wananchi kwa
kukubali kujumuika pamoja katika hafla hiyo na kumwomba Mzee Mgaya aendelee kuwapa
mwongozo wa namna ya kuenenda katika maisha.
Askofu Mkuu
wa Kanisa la Kilutheli Tanzania (KKKT) Alex Malasusa aliwaomba watanzania kuwa na
moyo wa unyenyekevu na kujitolea kulitumikia taifa katika utumishi wao kama ilivyokuwa
kwa IGP mstaaafu Mzee Mgaya.
Wageni wengine
waliohudhuria hafla hiyo ni Waziri wa Habari na Utangazaji Fenera Mukangara, Katibu
Mkuu Msaaafu wa Jumuiya ya Afrika Mashariki, Balozi Bakari Mwapachu, Balozi Antoni
Nyaki na wazee wengine maarufu kama Timothy Msangi.
Baadhi ya waumini mbalimbali wakiwa nje baada ya Ibada
 Mkuu
wa Jeshi la Polisi nchini (IGP) Mstaafu Philemoni Mgaya akiwa katika siku ya kumbukumbu ya kuzaliwa kwake
 Keki
Waziri  Mkuu
Mstaafu Cleopa Msuya akimpongeza aliyekuwa IGP Philemoni Mgaya
 Mzee Timothy Msangi akieleza Historia fupi ya IGP Mstaafu Philemoni Msangi
 Askofu Mkuu
wa Kanisa la Kilutheli Tanzania (KKKT) Alex Malasusa akitoa salam za Pongezi kwa IGP mstaafu

0 comments:

Post a Comment