
Kamanda wa Polisi Kanda Maalum ya Dar es Salaam, CP Suleiman Kova akizungumza na waandishi wa habari (hawapo pichani) “Wananchi wanatakiwa kuwa makini na hawa watu ni hatari sana,wamekuwa wakitoa namba zao za simu na kuwatangazia wananchi wanaotaka kujiunga nao ili wawe matajiri wapige namba walizotoa ili wajiunge baada ya kutoa fedha, nashangaa hata mimi watu wameshawahi kuniita Freemason wakati siyo kweli,” alisema Kamanda Kova.
Kamanda wa Polisi Kanda Maalum ya Dar es Salaam, CP Suleiman Kova, wiki iliyopita alifunguka kuwa, kuna watu wamekuwa wakimhusisha na imani ya Freemason.
Kamanda Kova aliyasema hayo alipokuwa akizungumza na waandishi wa habari kuhusu hali ya usalama wa mkoa wake kuelekea Sikukuu ya Krismasi na Mwaka Mpya.CHANZO CPL
0 comments:
Post a Comment