Nimekuwa nafuatilia kipindi cha asubuhi hii katika kituo cha TV cha StarTV. Nimewasikiliza wote. Huko Dar es salaam Dr. Kitila Mkumbo kaonesha upeo wake katika hili na Mwanaharakati Lenatus Mkinga ameonesha uwezo wake.
Kilicho nishangaza leo Kitila amepwaya sana kwa kutoa hoja zisizo na mashiko kwa kuegemea kumponda Dr. W. P. Slaa kwa kumwita hana adabu kwa kutokubaliana na matokeo hayo ambayo yamempa ushindi Edward Lowasa.
Kitila ameonesha kutokuegemea upande wowote pale alipotamka wazi kuwa utafiti huu una lengo la kumshafisha mtu fulani na ndiyo maaana watu walifanya sherehe ya kupongezana. Kaenda mbali na kutaja kuwa kundi hilo lililosherehekea ndilo hilo hilo lililompatia Dora 2500 cash ili aandae kipindi kwenye TV kwa lengo la kumsafisha mtu wao.SOMA ZAIDI>>>

0 comments:
Post a Comment