LEMUTUZ

Tuesday, November 4, 2014

LE MAJANGAZ WAREMBO DAR WALIVYONYONGWA

Posted by Williammalecela.com on Tuesday, November 04, 2014
DUNIA hii basi tena! Ni tukio la kusisimua ukilisoma mwanzo hadi mwisho lakini ni la kikatili sana! Ni lile la ndugu wawili warembo, dada na mdogo wake kukutwa wamekufa kwa kunyongwa ndani ya nyumba aliyokuwa amepanga mmoja wao huku muuaji akidaiwa alivaa taulo lenye weupe wa kufifia akitokomea zake.
Tukio hilo la kusikitisha lilitokea hivi karibuni kwenye Mtaa wa Mji Mpya, Kata ya Azimio wilayani Temeke jijini Dar es Salaam ambapo warembo hao, Mariam Buruhani (39) na dada yake Nuru Tumwaga (42) (pichani) walikutwa wamekufa katika nyumba hiyo aliyopanga Mariam.
Uwazi kama lilivyo kawaida yake, baada ya kuipata taarifa za kuwepo kwa vifo hivyo vya usiku mmoja, lilianza kufuatilia hatua kwa hatua.Kwa mujibu wa ndugu mmoja, mchana wa kuelekea siku ya tukio ambayo ni Jumamosi usiku, marehemu wote walionekana wakiwa wazima wa afya ambapo Mariam alikuwa kwenye saluni yake ya kike na Nuru akiendelea na shughuli zake  za kuwaremba wanawake wenzake.

Ikadaiwa kuwa, nje ya saluni ya Mariam kulikuwa na gari dogo jeusi ambalo huwa linapaki maeneo hayo kila wakati ikisemekana mmiliki wake ni bwana wa Mariam ambaye jina halikufahamika mara moja.
Email ThisBlogThis!Share to XShare to Facebook
Newer Post Older Post Home

0 comments:

Post a Comment

Subscribe to: Post Comments (Atom)

TOTAL PAGEVIEWS

Popular Posts

  • LIVE: RAIS MAGUFULI ANAKABIDHIWA RIPOTI YA UCHUNGUZI WA MADINI
  • BREAKING NEWZ: BASI LA NGANGA LATUMBUKIA MTARONI KULIKWEPA LORI
  • THE UDAKUZ: WEMA SEPETU Vs WOLPER!!
  • IRAN NA MAREKANI WAZIDI KUIMARISHA UHUSIANO
  • PICHA YA KWANZA YA KANISA LA ASKOFU MTATA GWAJIMA BAADA YA KUKUMBWA NA BOMOA BOMOA YA SERIKALI JANA LIVE.
Copyright © LEMUTUZ

Developed by MKCT