
Mama mzazi wa Wema Sepetu, Miriam SepetuHII ni mara yangu ya tatu nazungumza na mama mzazi wa Wema Sepetu, Miriam Sepetu juu ya mwenendo wake kwa mwanaye, ambaye ana simulizi nyingi zinazomhusisha na mambo yaliyo nje ya fani yake ya uigizaji.
Wakati ule, ilikuwa ni juu ya tabia yake ya mara kwa mara ya kulizungumzia penzi la Wema na Diamond, kabla wawili hao hawajaachana kwa mara ya kwanza. Alikuwa akimpinga waziwazi kijana yule wa Tandale, kwa madai kuwa anampotezea muda mwanaye na mambo mengine kama hayo.
Nilijaribu kumweleza kwa jinsi gani ilikuwa haipendezi kwake kufuatilia sana mambo ya kimapenzi kwa watoto, maana ingawa anayo nafasi kubwa, lakini
aina ya maisha ya siku hizi yanatoa nafasi kubwa zaidi kwa wahusika kuliko wazazi.Lakini wakati akijipongeza kwa kufanikisha kuachana kwa wawili hao, ghafla wakarudiana na kumfanya mama mtu kuaibika, kwani ilionyesha wazi mwanaye alikuwa bado ana mapenzi kwa Baby wake, Diamond Platinumz.
0 comments:
Post a Comment