Liberatusi Mwang'ombe akihutubia wanafunzi shule ya secondary Montfort iliyopo Rujewa, Mbarali
Akiongea
na watahiniwa wa kidato cha nne siku mbili kabla ya mtihani wa Taifa
2014, shule ya secondary Montfort iliyopo Rujewa, Mbarali,
Mwana-diaspora na "alumni" wa Montfort kutoka Washington, D. C.,
Marekani, Liberatus Mwang'ombe "Libe" alianza kwa kusema, Montfort ni
shule aliyo soma na anajisikia faraja akiyaona mazingira yale.
Aliendelea kwa kusema, maamuzi ya mwisho ya kila binadamu yapo chini ya
himaya yake. Alisema "huwezi kutegemea mtu baki au mwingine aongoze au
arutubishe maisha yako, ni wewe binafsi unaweza kufanya tofauti kwenye
maisha yako na kila binadamu ni kiongozi. Pia alisema anaamini kuwa kila
binadamu ana ndoto zake kwenye maisha; alisema; "ni muhimu kujiwekea
malengo ya ndoto zenu. Malengo ambayo yanatimilika, malengo ya
kiuhalisia na malengo yenye muda maalumu." Aliendelea na kusema, "ndoto
bila malengo itaendelea kuwa ndoto na kutimilizwa kwake kutaendelea kuwa
ni ndoto tu." Mwisho Ndg. Libe aliwaomba wanafunzi hao wasimuangushe
kwa kuweka malengo kwenye ndoto zao na kuhakikisha wanazitimiliza.
Mbali ya maongezi Ndg. Liberatus alichangia miundombinu ya elimu kwa wanafunzi hao
Moja ya wanafunzi akimshukuru Liberatus kwa kukumbuka alipotoka
Kwa habari zaidi za Liberatus Bagasa Mwang'ombe BOFYA HAPA
0 comments:
Post a Comment