Hili ndilo sanuku lililouhifadhi mwili wa Mwandishi/Mchambuzi wa Jukwaa Maalumu la MWALE WA DEMOKRASIA katika Gazeti la Raia Tanzania (Gazeti dada la Raia Mwema), kila Alhamisi. Mwili wa shujaa huyo wa Demokrasia uliswaliwa katika Kanisa Katoliki Msimbazi Jijini Dar es Salaam leo.
Ndugu wa marehemu Robert Lengeju wakitoa heshima za mwisho kwa mwili wa mdogo wao.
Heshima za mwisho ziliendelea kutolewa na ndugu jamaa na marafiki.
Godfrey Dililunga kutoka kampuni ya Raia Mwema wachapaji wa gazeti la Raia Mwema na Raia Tanzania akitoa heshima za mwandishi huyo wa Makala za Mwale wa Demokrasia katika gazeti lao.
Waombolezaji wakipita kutoka heshima za mwisho.
Mkuu wa Mkoa wa Mstaafu, Isdore Shirima nae alikuwepo kutoa heshima za mwisho kwa Lengeju.
Waombolezaji
wanakwaya wakiimba katika misa hiyo.
wanafamilia wakiwa Kanisani katika misa.
Wanafamilia, ndugu jamaa na marafiki wakiwa katika misa hiyo leo.
Kaka wa Marehemu Charles Lengeju akiwa amebeba msalaba wa marehemu.
Gari lililobeba mwili wa marehemu Robert Lengeju likiwa tayari kwa safari ya Kipera Mkoani Morogoro.
0 comments:
Post a Comment