Tuesday, November 4, 2014

Nikki-wa-Pili
Msanii msomi na msemaji mkuu kutoka kundi la Weusi Nikki wa pili, amewajia juu kundi la vijana wanaosadikiwa kufanya fujo katika mdahalo wa pili ulioandaliwa na taasisi ya  Mwalimu Nyerere ili kuielewa kwa kina katiba inayopendekezwa kama ilivyopitishwa na bunge maalum la katiba
.
Kongamano hilo lililofanyika jana ndani ya ukumbi wa Blue Pearl, Ubungo Plaza liliingia dosari na vurugu kubwa mpaka kupelekea polisi kuingilia kati na kutuliza fujo hizo kwa mabomu ya machozi, baada ya kundi la vijana kusadikiwa kuanzisha fujo huku wakiwa na mabango mbali mbali, wakiimba CCM,CCM,CCM na “Kama sio juhudi zako Nyerere Warioba angekuwa wapi na kuhamia jukwaani kuendeleza fujo hata kupelekea kusitishwa kwa kongamano hilo
Kutokana na hali hiyo kutokea, Nikki ameandika ujumbe huu kwa vijana kupitia acc yake ya Instagram akilaani kitendo alichofanyiwa Warioba
Credit : Dj Fetty
T

0 comments:

Post a Comment