Wednesday, November 26, 2014

Uamuzi huo ulipokewa kwa hisia tofauti, upande wa IPTL ukishangilia kwa kupewa ulinzi, huku baadhi ya watu wakieleza kuwa Mahakama imezuia mjadala huo unaosubiriwa kwa hamu.Muda mfupi baada ya hukumu hiyo kutolewa na kusambaa kwenye vyombo vya habari na mitandao ya kijamii, Mwenyekiti wa PAC, Zitto Kabwe ambaye pia alikuwa mdaiwa, aliandika katika ukurasa wake wa Twitter, “Mahakama imetoa zuio la kujadili taarifa ya CAG kuhusu Escrow. Hata hivyo, PAC itawasilisha taarifa yake kwa mujibu wa ratiba ya Bunge hapo kesho.” Mkurugenzi wa Shughuli za Bunge, John Joel alisema: “Sisi hatuna taarifa hizo kutoka mahakamani, ratiba ya Bunge inaendelea kama kawaida.” >>>>

0 comments:

Post a Comment