Ukiangalia kama ‘Mdogo Mdogo’ ilikuwa inazungumzia mapenzi hayaulizi kwanini so ilikuwa lazima ioneshe pande mbili, kuna wazungu na mimi ni mwaafrika na familia yangu ya kiafrika. Kuna mtoto wa kizungu ambaye ananizimia mimi mwaafrika lakini familia yake haipendi ukizingatia wao ni wafalme na nini. Lakini mtoto bado ananipenda hivyo hivyo, ananifuata mpaka porini ananikuta kwenye maji naimba mimi kule. Mpaka dakika ya mwisho anakuja baba yake anamkuta yupo kwetu kijijini anacheza na familia yetu sisi so dakika ya mwisho unakuta mzee mwenye anakubali mwanae aolewe.
Kiukweli amejitahidi na amefanya vizuri sana. Bado tunawasiliana, hata juzi nilimtumia meseji nikamwambia ‘Melissa natamani ujue jinsi gani unazungumziwa, nikasema ‘najua kabisa huko South Africa hawawezi kuwa wanaizungumzia hii video kama wanavyoizungumzia hii video huku nyumbani, natamani ujue jinsi gani walivyokupokea, natamani ujue umefahamika kiasi gani.>>>

0 comments:
Post a Comment