Tuesday, November 11, 2014

 Kutoka kushoto waliokaa  Mwenyekiti wa Halmashauri ya Mji wa Njombe Bw. Edwin Mwanzinga, Mkuu wa wilaya ya Njombe Bi Sarah Dumba, Kaimu Mkurugenzi wa Halmashauri Bw. Tadeo Kabonge na Kaimu Mkurugenzi wa Tassaf Taifa Bw. Peter Luanda wakiwa kwenye picha ya pamoja na madiwani wa kata za Halmashari hiyo waliosimama, Picha zote na  James Festo.
  Kaimu Mkurugenzi wa Halmashauri ya Mji wa Njombe Bw Tadeo Kabonge akizungumza kabla ya kufunguliwa kwa warsha hiyo
Mkuu wa Wilaya ya Njombe Bi Sarah Dumba akifungua Warsha ya siku moja ufunguzi wa Warsha ya Tasaf inayoendelea mjini Njombe


Na James Festo, Njombe.

Wawezeshaji wa mradi wa  kunusuru kaya masikini unaoendeshwa na mfuko wa maendeleo ya jamii (TASSAF) awamu ya tatu wenye lengo la kuwakwamua wananchi wa kipato cha chini wametakiwa kutowapendelea ndugu zao katika utekelezaji.


Akifungua warsha ya siku moja Mkuu wa Wilaya  wa Njombe  Bi.Sara Dumba  ya kuwajengea uelewa wawezeshaji wa mradi huo kuhakikisha unawanufaisha walengwa ambao ni familia zenye hali duni ya maisha na  watoto ikiwa ni utatuzi wa changamoto zilizojitokeza katika utekelezaji wa TASSAF awamu mbili za awali.


“Tunashukuru serikali  kwa kutuchagua kuwa miongoni mwa watakaoanza kunufaika kwa niaba ya wananchi tumeupokea, sasa kazi kwenu wawezeshaji msije mkaanza kupendelea…unampa msaada kwa sababu ni ndugu yako….ni mjomba wako, kinachotakiwa  mradi uwanufaishe wale waliolengwa tu sio watu wengine” alisema Bi Dumba.

Kwa upande wake Kaimu Mkurugenzi wa Tassaf Taifa Bw. Peter Luanda  alisema umelenga kuzifikia kaya milioni moja ambazo zinaishi katika mazingira magumu na kwa awamu awamu ya kwanza utachukua maeneo machache kwa sababu bado wanafanya tathmini na baada ya kumalizika wataongeza vijiji vingine.


Alisema kuwa mradi huo umelenga kuboresha maisha , kutoa ajira kwa wenye uwezo wa kufanya kazi, kuboresha miundombinu ya maji, afya na elimu, kutoa ruzuku kwa familia maskini hasa akina mama wajawazito pamoja na watoto wenye chini ya umri wa miaka mitano.


Katika  hatua nyingine aliishukuru Halmashauri hiyo kwa mapokeo waliyoonyesha sambamba na kuchagua wawezeshaji watakao ungana na timu ya Tassaf  Taifa katika mradi huo.

Mradi huo huo uliozinduliwa agost 2012  Mkoani Dodoma na Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dk. Jakaya Kikwete, Utekelezaji wa mradi ukianza mwezi februali 2013 na lengo lake ni kutambua kaya masikini na umeanza na Halmashauri 16  Nchini na inatarajia kuzifikia zote 161.

0 comments:

Post a Comment