Posted by Williammalecela.com on Wednesday, November 05, 2014

 |
MAMBO ya urithi! MOJA ya nyumba mbili
zilizoachwa na marehemu Muhidin Maalim
‘ Gurumo’ , iliyopo Tabata jijini Dar es Salaam,
ambayo ndiyo anayoishi mkewe Pili Saidi, ipo
sokoni baada ya watoto wake kung’ ang’ ania
iuzwe.
Kwa mujibu wa chanzo cha kuaminika,
watoto hao wapatao sita , wamemlazimisha
mama yao huyo wa kambo kukubaliana nao
kuhusu jambo hilo, wakiahidi kumpatia fungu
lake, kwani wao wanataka kugawana mali
iliyochumwa na baba yao.
“Yule mama yupo kwenye kipindi kigumu
kweli , maana wale watoto hawana
ushirikiano naye kabisa , sijui ataishi kwenye
mazingira gani na sidhani kama wanampa
msaada wowote wa kujikimu
kimaisha,”kilisema chanzo chetu.
Bi . Pili alipoulizwa juu ya ukweli wa habari
hizo , alikiri nyumba kuwa njiani kuuzwa
kwani yeye hana uwezo wa kupingana na
watoto wa marehemu , hivyo amekubaliana
nao ili kujiepusha na mabalaa mengine.
“Ni kweli hii nyumba watoto wa marehemu
wote wamekubaliana kuiuza ili wagawane na
wameahidi kunipa fungu langu , siwezi
kupingana na hilo kwa kuwa mimi
sikubahatika kumzalia, japo sijui hatma ya
maisha yangu nitakapoondoka humu ndani
maana hawa vijana hatuna ushirikiano mzuri
kwa sasa .”
Alisema hata gari ya marehemu
aliyozawadiwa na Diamond ilitaka kuuzwa ,
lakini akasimama kidete kuitetea kwa kuwa
msanii huyo alimwambia kwa kuwa mumewe
amefariki basi itakuwa mali yake na kusema
inamsaidia kujikimu kimaisha kwani
anaifanyia biashara . |
0 comments:
Post a Comment