| Toka jana kumekuwa na habari za kutatanisha kuhusu Mwanamuziki maarufu nchini na Msanii wa bongo muvi Patcho Mwamba kuhusu kufumaniwa na mke wa mtu na kupigwa vibaya sana mpaka kufanyiwa mabaya zaidi. Ni habari iliyoeneea haraka sana kwenye mitandao ya kijamii na magazetini lakini leo imethibitishwea na Patcho Mwamba mwenyewe pamoja na Mwanasheria wake wa binafsi kwamba sio habari za ukweli. Ukweli ni kwamba Patcho Mwamba ana matatizo ya kuvimba sura kila anapokunywa pombe na hasa kali, jana aliamua mwenye kwa hiari yake kuiweka hii picha Instagram akiomba msaada wa kidaktari ili atafute dawa ya hilo tatizo lake sugu. Kuna wazushi walioamua kwa makusudi kuibadili hii habari na kuifanya kama ilivyotangazwa na karibu vyombo vyote vya habari nchini ni habari za uongo na hazina ukweli wowote! - Le Mutuz |
0 comments:
Post a Comment