Posted by Williammalecela.com on Monday, December 22, 2014
 |
JOHNSON LUKAZA WA KESI YA EPA ASHINDA KESI Na Happiness Katabazi
HATIMAYE Mahakama ya Hakimu Mkazi Kisutu Dar es Salaam, imemwachiria
huru Mwenyekiti wa Makampuni ya Proin, Johnson Lukaza na mdomo wake
Mwesigwa Lukaza waliokuwa wakikabiliwa na kesi ya wizi wa Sh.Bilioni
Sita Katika Akaunti ya Madeni ya Nje ya Benki Kuu(EPA), baada ya kumuona
Hana hatia Katika Kesi iliyokuwa ikimkabili. Hukumu hiyo Imetolewa Jaji wa Mahakama Kuu Edson Mkasimongwa aliyekuwa alisaidia na Hakimu Mkazi Pamela Mazengo.
Lukaza ambaye pia ni Mjumbe wa Baraza la Chuo Kikuu cha Bagamoyo (UB)
alikuwa akitetewa na Wakili maarufu nchini Alex Mgongolwa aliyekuwa
akisaidiwana na Wakili Alex Mshumbusi. Akisoma hukumu hiyo Jaji
Mkasimogwa alisema Kesi hiyo ya Mwaka 2008 , Mahakama imesikiliza
ushahidi wa pande zote mbili Na kupitia vielelezo mbalimbali, Mahakama
yake Imefikia uamuzi wa kuwaachiria huru washitakiwa wote Wawili
kwasababu upande wa jamhuri umeshindwa kuleta ushahidi thabiti ambao
ungeishawishi Mahakama hiyo iwakute na hatia washitakiwa Hao.
|
0 comments:
Post a Comment