Thursday, December 25, 2014

MNENGUAJI na kiongozi wa wanamuziki wa Bendi ya Extra Bongo ‘Wazee wa Kizigo’, Hassan Musa ‘Super Nyamwela’ ametoa ya moyoni na kusema kwamba pengo la Mwanaisha Mbegu ‘Aisha Madinda’ haliwezi kuzibika milele.
Mnenguaji na kiongozi wa wanamuziki wa Bendi ya Extra Bongo ‘Wazee wa Kizigo’, Hassan Musa ‘Super Nyamwela’.
Akistorisha nasi, Nyamwela alisema ameshawafundisha wanenguaji wengi kucheza kwani yeye ndiye mwalimu wao lakini hakuna mwanafunzi ambaye alikuwa anajua kunengua kama Aisha Madinda na alikuwa akimfurahisha kutokana na wepesi wake. 
“Mimi na Aisha tumetoka mbali sana, mimi ndiye niliyemfundisha kunengua tangu enzi hizo, kiukweli hakuna wa kuliziba pengo lake kwani alikuwa ni mwepesi kuelewa halafu alipenda sana kujituma jukwaani lakini ndiyo hivyo mipango ya Mungu hatuwezi kuipinga,” alisema Nyamwela.
Aisha Madinda alifariki ghafla wiki iliyopita na kuzikwa Kigamboni, jijini Dar ambapo kifo chake kimeacha utata mkubwa.

0 comments:

Post a Comment