Akizungumza na waandishi wa habari leo, katika
Ofisi Ndogo ya Makao Makuu ya CCM, Lumumba jijini Dar es Salaam, Katibu
wa NEC, Itikadi na Uenezi, Nape Nnauye amesema, kulingana na kosa
lililojitokeza kuwa la wazi hakuna haja ya kupoteza fedha na muda
kufanya uchunguzi kabla ya kuwachukulia hatua waliohusika.
"Kwa
mfano, Mkurugenzi wa Halmashauri ana kila kitu na alijua mapema kuwa
uchaguzi utafanyika lini kwa kuwa halikuwa jambo la dharura, inakuwaje
anaruhusu karatasi ziende kwenye vituo
zikiwa zimechapishwa hovyo au mahali pengine vifaa viwe vicheche?"
alihoji Nape na kuongeza "Sasa hapa unahitajika uchunguzi gani tena
kubaini aliyevurunda?".
"Mahali pengine zimefika karatasi za kupigia kura jina la mgombea wa CCM
nembo ya CUF, au mgombea wa CUF nembo ya CCM! huu ni uzembe wa hali ya
juu sana na adhabu yake haistahili kusubiri uchunguzi", alisema Nape.
Akizungumzia matokeo ya awali ya Uchaguzi huo, Nape alisema licha ya
vyama vya upinzani kuwa na umri wa miaka 22 sasa, huku vikifanya
harakati za kujaribu kuungana katika umoja wanaouita Ukawa, bado CCM
imewagaragaraza vibaya.
Nape amesema, katika uchaguzi huo , CCM
imepata zaidi ya asilimia 85 ya ushindi kwa nchi nzima, huku Dar es
Salaam, ikiwa na asilimia zaidi ya 75 licha ya kwamba Chadema wanao
wabunge wawili katika mkoa huo.
"Katika mazingira ya sasa ambayo
vyama vya upinzani vina miaka 22, na vinafanya hata harakati za kujaribu
kuungana, asilimia 85 si ndogo kwa CCM, na tunaamini huu ni mwanzo
mzuri, na hatuoni namna ambavyo asilimia hii itabadilika katika uchaguzi
mkuu mwakani, maana uchaguzi huu ni kama kura za maoni", alisema Nape.
"Wanaosema, asilimia ya CCM imeshuka, wajue kwamba tuliposema tunataka
mfumo wa vyama vingi maana yake tulitaka ushindani katika demokrasia.
Katika demokrasia ya ushindani ni vema kuruhusu vyama vya upinzani
vikakua ili ushindani huo uonekane", alisema Nape.
"Hata hivyo
inasikitisha kwamba licha ya vyama vya upinzani kuwa na umri wa miakaa
22 sasa, bado havijaweza kujenga imani ya kutosha kwa Watanzania hata
kufikia asilimia 40 kuwa vinaweza kuongoza, lazima wapinzania wazidi
kujijenga ili Watanzania wawaamini, asilimia hii 14 waliyopata karika
uchaguzi huu wa serikali za mitaa bado ni ndogo sana kwa uhai wa miaka
zaidi ya 22".
Nape aliwashukuru wananchi nchini kote kwa
kuendelea kuiamini CCM, na kuchagua wagombea wake, huku akivipongeza
vyama vya upinzani kwa maeneo waliyochaguliwa, akiwataka kuchapa kazi
vinginevyo siku za baadaye wananchi watawahukumu kwa kuwatosa
|
0 comments:
Post a Comment