DIRECTORATE OF PRESIDENTIAL COMMUNICATIONS
Telephone: 255-22-2114512, 2116898
E-mail: ikulucommpress@googlemail.com
Website : www.ikulu.go.tz
Fax: 255-22-2113425
PRESIDENT’S OFFICE,
STATE HOUSE,
1 BARACK OBAMA ROAD, 11400 DAR ES SALAAM.
Tanzania.
TAARIFA KWA VYOMBO VYA HABARI
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mheshimiwa Dkt. Jakaya Mrisho Kikwete amemteua Bwana LaurenceNyasebwa Mafuru kuwa Msajili wa Hazina kuanzia tarehe 5 Novemba, 2014.
Taarifa iliyotolewa leo Desemba 11, 2014 na Katibu Mkuu Kiongozi, Balozi Ombeni Y. Sefue inasema kuwa kabla ya uteuzi wake, Bwana Mafuru alikuwa Mkuu wa Idara ya Rasilimali Fedha katika Ofisi ya Rais inayohusika na ufuatiliaji Miradi ya Matokeo Makubwa Sasa (PDB). Aidha Bwana Mafuru pia alikuwa Kaimu Mtendaji Mkuu wa Benki ya FBME iliyowekwa chini ya uangalizi wa muda wa Benki Kuu ya Tanzania (BoT).
Wakati huohuo, Taarifa ya Balozi Sefue inasema Rais Kikwete amemteua Bibi Beng’i Mazana Issa kuwa Katibu Mtendaji wa Baraza la Taifa la Uwezeshaji Wananchi Kiuchumi kuanzia tarehe 4 Desemba, 2014. Kabla ya uteuzi wake, Bibi Mazana Issa alikuwa Mkurugenzi wa Utawala wa Fedha katika Tume ya Kudhibiti UKIMWI (TACAIDS).
Imetolewa na:
Kurugenzi ya Mawasiliano ya Rais,
Ikulu – Dar es Salaam
0 comments:
Post a Comment