Nyumbani kwa muigizaji wa filamu, Wema Sepetu, kumetokea tukio la kushangaza la watu wawili wanaodaiwa kuwa mafundi, kupigwa na kudhalilishwa kwa kuachwa uchi wakidaiwa kuhusika na wizi.
Kwamujibu wa Bongo5.com ambao walizungumza jana na jirani wa Wema aliyetambulika kwa jina la Mama Steve, alisema tukio hilo lilitokea Ijumaa majira ya saa 5 asubuhi mpaka saa 9 jioni.
“Waliopigwa na kulazwa chini uchi wa mnyama ni mafundi ambao wanakujaga kila siku kumtengenezea Wema nyumba yake,” amesema mama huyo. “Sasa baada ya kumaliza kazi yao wakaondoka, baada ya kuondoka wakaitwa tena na kuambiwa kuna simu imeibiwa ndani, ndo mtiti ukaanza.”
“Petit akatumwa akachukue mabaunsa 7 na baada ya kufika wakapandisha muziki mpaka mwisho ili sisi tusisikie nini kinaendelea huko ndani. Sasa kuna mtu alikuwa anapita hapa kwenye geti lao akasikia mtu analia sana ikambidi akachungulie ndo akamkuta fundi watu wawili wamelazwa chini uchi wa mnyama wanapigwa na hawana nguvu kabisaSOMA ZAIDI>>>

0 comments:
Post a Comment