Mkurugenzi wa Bendi ya Double M Sound, Muumini Mwinjuma ‘Kocha wa Dunia’. KURUGENZI wa Bendi ya Double M Sound, Mwinjuma Muumini ‘Kocha wa Dunia’, amefunguliwa kesi kwa jalada namba; NJ/RB/4150/2014 madai KUTOKUWEPO ENEO LA TUKIO na kukiuka masharti ya mkataba ya kufanya shoo mkoani Njombe. Mwandaaji wa shoo hiyo iliyofanyikia Ukumbi wa Day to Day, Sylvia Mwakkikufi akizungumza na Amani juzi, alisema amefanya hivyo baada ya Muumini na bendi yake kutokea ukumbini saa nane usiku Jumamosi iliyopita akiwa na kufanya shoo kwa dakika 35 tofauti na muda wa mkataba.
Muumini Mwinjuma akiwa kazini.“Licha ya kuchukua pesa yangu na kutofanya kazi, kapoteza muda wangu, kanishushia hadhi, kanikosanisha na wadhamini,” alisema. Sylvia ambaye ni mwandaaji wa shoo mbalimbali mkoani Njombe hivi karibuni aliandaa shoo na kuiita Usiku wa Watoto Yatima.
Hata hivyo, asubuhi yake, Sylvia alisema, Muumini alikamatwa na Polisi wa Njombe na kuwekwa lupango kwa siku mbili kabla ya kudhaminiwa. Kesi yake itatinga mahakamani wakati wowote.

0 comments:
Post a Comment