Imeripotiwa kuwa baada ya mshiriki wa Nigeria kwenye shindano la Big Brother Afrika, Tayo kuzikosa dola laki tatu za Biggie zilizomwendea Idris wa Tanzania Jumapili iliyopita, mshiriki huyo wa Naija amezawadiwa $350,000 sawa na zaidi ya milioni 600 kutoka kwa shabiki wake bilionea.
Bilionea huyo aitwaye Ayiri Emami ameamua kuongeza dola 50,000 juu zaidi ya ile ambayo ilitolewa na Biggie ambayo ni $300,000 kutokana na kuwa shabiki mkubwa wa Tayo.
Staa wa Nigeria Davido ameshare picha ya story hiyo Instagram na kuandika "we do this easy, bar dey".
Inasemekana hii si mara ya kwanza kwa bilionea huyo kumwaga mkwanja mrefu kwa wasanii anaowapenda, aliwahi kufanya hivyo kwenye harusi ya 2Face 2010 ambapo inasemekana alitoa zaidi ya Naira milioni 20 (sawa na zaidi ya Tsh 189,000,000) na kumzawadia Range Rover mpya, na pia alimzawadia msanii mwingine aitwaye Durella gari aina ya Toyota Prado Jeep.
=======================
Mnigeria Tayo alitoka mikono mitupu #BBAHotshots 2014, Bilionea kampa fungu hili Nigeria
![]()
Mshiriki wa BBA Hotshots 2014 kutoka Nigeria, Tayo Folarin.
Baada ya East Africa yote kuinua shangwe kubwa siku ya Jumapili Desemba 7 kusherehekea ushindi wa nguvu alioupata Mtanzania Idris kwenye BBAHotshots, kulikuwa na story kwenye mitandao ya kijamii ambazo hazikuwapendeza watu wengi kwani ilionekana kama baadhi ya watu kama Nigeria hawakuwa na amani kuukosa ushindi huo na kuuona ukija Tanzania.
Sasa mpya kutoka Nigeria ni kwamba bilionea mmoja hakupendezwa kumuona mwakilishi wao Tayo akiambulia patupu, bilionea huyo Ayiri Emami amempatia Tayo Folarin pesa ambazo ni zaidi hata ya kiwango ambacho kimetolewa na BBAHotshotskwa mshindi wa kwanza.
Tunawafahamu mabilionea wachache kutoka Nigeria wakiongozwa na Aliko Dangote,Emami leo anakaa kwenye headlines karibu zote za Nigeria kwa kumpatia Tayo dola laki tatu na nusu (350,000/=)
Bilionea Ayiri Emami
Kiasi hicho ni backup kwa Tayo ambaye alionekana mnyonge sana usiku ambao Idris alitangazwa mshindi, hii itampa Amani ya kuendelea maisha na mpenzi wake na mtoto wake mmoja ambaye alizaliwa wakati Tayo akiwa ndani ya Jumba la Big Brother.
Wednesday, December 10, 2014
Subscribe to:
Post Comments (Atom)
0 comments:
Post a Comment