rais wa korea kasikazini
uchambuzi kutoka kwa Ben wa saanane
Sasa huyu Dogo(Rais kijana 32Yrs Old) wa Korea ya Kaskazini anaelekea kuvuka mipaka. Nilipenda jinsi walivyosimama kidete kama mshirika Muhimu wa Mrengo wa Kushoto sambamba na China kule Mashariki ya Mbali kuleta Uwiano wa nguvu ya madola lakini sasa mhhh! Huu Udikteta umepindukia.Kwa hali hii nimepata wasiwasi sana...!
Kwanza Mwaka Huu aliamrisha Wanaume wote wanyoe Panki/Kiduku kama yeye nchini mwake
Sasa baada ya kumnyonga mjomba wake aliyekua Kiongozi wa juu mwenye nguvu serikalini kwa tuhuma za kutaka kumpindua imedhihirika pia watu wote wenye jina linalo fanana na la kwake wabadilishe haraka
Hawataki jina linalofanana na Rais Kim Jong-Un wa Korea ya kaskazini amiri jeshi mkuu wa jeshi lenye wanajeshi zaidi ya Milioni moja na mkuu wa nchi ambaye asilimia kubwa ya bajeti ya nchi inaelekezwa katika kujiimarisha kijeshi ,kwamba bora wafe njaa lakini wailinde nchi na misimamo yao mikali kwa kuimarisha Jeshi na idara ya ujasusi kukabiliana na maadui wa nje hasa korea ya Kusini washirika wakubwa wa Marekani waliotengana nao mwanzoni mwa vita baridi katika vita yao 1950-1953 na kugawanyika Kusini(Pro-western) na Kaskazini(Pro-East yaani SOVIET na washirika wake)
Kwa hiyo vyeti vya kuzaliwa na hata vyeti vya shule na vyuo vya watu wenye jina kama hilo sasa vinatakiwa kubadilishwa.Mamlaka ya polisi na taasisi nyingine ziliagizwa kufanya hivyo mwaka mmoja kabla hajaingia madarakani
Na imekatazwa kuwa hakuna kulalamika wala kueneza uvumi hadharani kuhusu hatua hiyo.Itakua unakaribisha hali ya uhaini(Treasonable state).
Hali hii imenifanya nimkumbuke yule mbunge Viti Maalumu anayetumia jina la Nyerere licha ya kutokua na uhusiano na familia ya Nyerere kwa sasa jinsi anavyoongea pumba huku akitumia jina hilo kujinufaisha kisiasa
0 comments:
Post a Comment