Posted by Williammalecela.com on Tuesday, December 23, 2014
Kwanini Waziri Tibaijuka ni lazima ajiuzulu sasa au aondolewe na Mh. Rais
- Jana kwenye Press Conference yake amesema mengi sana lakini
hakuna la maana wala msingi alilolisema la kumnusuru na hasa baada ya
Mwanasheria Mkuu Werema ambaye hakutajwa kupokea senti tano za Escrow
alipotangulia mwenyewe badala ya kumsubiri Rais kama anavyotaka kufanya
Waziri Tibaijuka, ninasema hivi:-
1. Waziri alikuwa UN kwa muda mrefu sana anajua maadili ya UN kwamba
ukituhumiwa tu kupokea hata senti tano nje ya kazi yako unafukuzuwa kazi
siku hiyo hiyo, ndio maana Ban Ki Moon amesema haamini kwamba ni kweli
kuwa Waziri Tibaijuka amepokea hizo pesa. Now understand hakusema
haamini kwamba ameiba isipokuwa haamini kwamba amepokea hizo pesa, WHY?
anajua kwamba huyu Mama baada ya muda wote aliokuwa UN anajua better
kuhusu kupokea anything nje ya kazi.
2. Waziri Tibaijuka jana kuna kosa moja kubwa sana alilolifanya nalo ni
kutooonyesha the media record ya tabia yake ya kupokea pesa za misaada,
alitakiwa awaonyeshe waandishi wa habari historia yake ya kupokea
misaada akiwa Waziri na kabla hajawa Waziri at least angekuwa na upenyo
wa kutokea kwamba ni tabia yake toka akiwa UN kupokea misaada ya pesa
kutoka kwa wafanyabiashara wakubwa sio hapa tu hata alipokuwa huko UN.
Sasa kwa kushindwa kuonyesha hilo anakuwa anaelea elea na utetezi wake
kwamba zilikujwa ni pesa za misaada ya Shule.
3. Pesa za Escrow alizozipokea kuna Makanisa na MaaAskofu waliozikataa,
kwa mfano Kanisa la Saint Peters lilizikataa pesa hizo meaning kwamba
Kanisa lilishituka kwamba process haiko sawa sasa ina maana Kanisa
linaweza kuwa na smart judgement kuliko Professor Anna Tibaijuka WAziri
wa Jamhuri na former UN Boss? Haingii akilini, uchunguzi ulkiofikishwa
bungeni umeonyesha Waziri alipokea pesa hizo 1.6 Billion na kuziingiza
kwenye account ya shule anayioisema na siku mbili later akazitoa bila
Shule kujua wala kuidhinishwa na bodi ya Shule WHY?
- Kwa kumalizia nasema hivi Waziri Tibaijuka aondoke sasa kabla ya Rais
hajamuondoa maana hawezi kumuacha no way itakuwa ni Banana Republic
Taifa ambalo Mawaziri wanaruhusiwa kupokea Billions kutoka kwa wafanya
biashara bila kumuarifu anybody are you kidding me or what? Nashangaa
mpaka sasa nafsi yake haimsuti kwamba MWanasheria Mkuu ambaye hakupokea
senti tano amejiondoa mwenyewe kuwajibika na yeye aliyepokea anadai hana
makosa please, enough Wananchi wamechishwa na hizi longo longo huyu
mama kuna mnaoheshimiana naye mnasoma hapa mwambieni alichokifanya jana
kwenye media ni sawa sawa na ile Press ya Miss Tanzania nothing personal
lakini hata hiki Chama Cha Mapinduzi mnakimaliza wenyewe I mean Mjumbe
wa Kamati Kuu ya CCM ya Nyerere usikike umepokea Billion kutoka mfanya
biashara hivi kweli kungekuwa na kesi tena? Alikuwa anasema nini pale
mtumzima mwenye elimu kubwa kuliko Wananchi wengi wa Taifa hili? Halafu
na nyie media ya bongo kwa nini huwa hamuulizi maswali serious?
- Alipokuwa anawataja kina Rais Mkapa na Mzee Mengi kuwahi kumchangia
mngemuuliza alipokuwa UN aliwahi kuchangiwa na je kabla hajwa Waziri
Mkapa na Mengi waliwahi kumchangia?
- MAMA TIBAIJUKA JIUZULU TU UKINUSURU CCM CHAMA CHA MAPINDUZI HUWEZI
KUWA MJUMBE WA KAMATI KUU YA CCM NA WAZIRI WA JAMHURI UKAANZA KUPOKEA
MISAADA YA WAFANYA BIASHARA WAKUBWA NCHINI NI MAKOSA MAKUBWA SANA
JIUZULU NOW, IFIKE MAHALI VIONGOZI WA TAIFA MCHAGUE KUWA VIONGOZI AU
KUPOKEA MISAADA YA WAFANYA BIASHARA WAKUBWA ILA HAMUWEZI KUCHANGANYA
VYOTE, HAPANA SISI WANANCHI HATUTAWARUHUSU!!
Le Mutuz
0 comments:
Post a Comment