Sitti Mtemvu Katikati akiwa na washindi wenzake katika shindano la mwaka 2014
Shindano la Miss Tanzania limesimamishwa kwa muda wa misimu miwili ili kutoa fursa kwa waandaaji wa shindano hilo kurekebisha baadhi ya kasoro ambazo zimekuwa zikilalamikiwa mara kwa mara. Kaimu Katibu Mtendaji wa Baraza la Sanaa la Taifa Godfrey Mngereza amesema kuwa serikali kupitia baraza hilo imefikia umamuzi huo kutokana na malalamiko ya mara kwa mara kutoka kwa wadau mbalimbali na wapenzi wa shindano hilo.
Amesema
imefika wakati sasa waandaji warekebishe masuala kadha ili kuondoa
malalamiko na manung'uniko miongoni mwa wadau ili kulipa heshima
shindano hilo, pia liweze kuheshimika na kila mtu Mngereza
ameongeza kuwa, serikali kupitia wizara ya Habari, Vijana, Utamaduni na
Michezo imelipa dhamana baraza hilo kisheria kushughulikia masuala yote
yanahusu sanaa na Utamaduni hivyo baraza hilo lina mamlaka ya kuingilia
kati endapo litajiridhisha kuwa kuna masuala hayaendi sawasawa.
Kuhusu
masuala wanayotakiwa kuyarekebisha, Mngereza amesema kuna mambo mengi
hayako sawa katika mchakato mzima kuanzia katika ngazi ya vitongoji, na
baraza limekuwa likipata malalamiko karibu kila mwaka lakini kwa mwaka
huu malalamiko yamekuwa mengi zaidi.
Mngereza
amesema “Kama imefikia wakati hadi mshindi wa shindano mwenyewe
analazimika kuvua taji lake kwa shinikizo, ina maana kuna tatizo,
kwahiyo tumewapa muda ili wakaangalie upya mchakato mzima na wafanye
marekebisho”
Kupitia
mtandao wa kijamii wa Instagram, William Malecela (Le Mutuz) ambae pia
ni mmoja wa waandaji wa shindano la Miss Ilala amekua na haya yakusema
baada ya Miss Tanzania Kufungiwa miaka 2...
0 comments:
Post a Comment