Mfanyabiashara milionea maarufu wa Moshi, Augustino Mallya (40) aliyejiua kwa risasi. Baadhi ya watu waliokuwa katika msiba huo walikuwa wakisikika wakisema kuwa msiba huo unaweza kuwa na mambo ya kishirikina kwa sababu vifo vya wafanyabiashara hao wawili mmoja akiwa na makazi Arusha, vinafanana na vina utata.
MWEZI mmoja baada ya mfanyabiashara wa Arusha, Timoth Mroki (36) kujiua kwa kujipiga risasi, mfanyabiashara milionea mwingine maarufu wa Moshi, Augustino Mallya (40), naye Jumatatu iliyopita alijiua kwa kujipiga risasi akiwa nyumbani kwake eneo la Karanga, mjini Moshi huku ushirikina ukitajwa.
“Kuumwa siyo kifo, inawezekana wamechezewa na wabaya wao ndiyo maana wote wamejiua kwa risasi na kusababisha viongozi wa dini kushauri kwa kusema hili tuliangalie,” alisema muombolezaji mmoja kwa sharti la kutotajwa jina lake gazetini. Milionea huyo alikuwa akijishughulisha na biashara za maduka ya bidhaa za jumla na nyumba za kupangisha katika eneo hilo la Karanga.BOFYA INAENDELEA>>>
0 comments:
Post a Comment