Posted by Williammalecela.com on Friday, December 12, 2014
Habari ya mjini! Gumzo katika ulimwengu wa mastaa Bongo ni kitendo cha mkali wa muziki wa Kizazi Kipya, Nasibu Abdul ‘Diamond Platnumz’ kuendelea kujiachia na staa wa mrembo mwenye maskani yake nchini Uganda na Afrika Kusini ‘Sauz’, msanii Zarinah Hassan ‘Zari’ au ‘The Boss Lady’ huku aliyekuwa ‘kiburudisho’ wa jamaa huyo, Wema Isaac Sepetu ‘Beautiful Onyinye’ akijibu mapigo kwa kumnasa mwigizaji Joseph Van Vicker wa Ghana, Ijumaa lina sarakasi nzima.
Wema Isaac Sepetu ‘Beautiful Onyinye akimbusu Van Vicker kimahaba. WEMA ATIMKIA GHANA
Wakati Diamond akitimkia Marekani kwenda kutumbuiza kwenye sherehe za 53 za Uhuru wa Tanganyika kwa Wabongo waishio nchini humo (Diaspora), Desemba 9, mwaka huu, Wema yeye alitimkia kwenye Mji Mkuu wa Ghana jijini Accra kuungana na Van Vicker kwa ajili ya ‘projekti’ kama ilivyokuwa kwa Diamond na Zari. SOMA ZAIDI>>>
0 comments:
Post a Comment