Friday, January 2, 2015

Ninayoandika hapa ni panya road kinondoni na mwananyamala muda huu wanafanya yao
======== UPDATES =======

- Panya Road wamevamia maeneo mengi Dar... Kijitonyama, Mwanyamala, Kinondoni ni vurugu tupu; risasi na mapanga


- Baa za Meridians, Jakaranda na Mango zimefungwa

- Baa ya Catalunya huko Sinza inadaiwa imevamiwa pia


Quote By godimpare View Post
baada ya kumzika mwenzao aliye uwawa jana na sungusungu sasa leo wamemzika mwenzao huku wakijeruhi watu na kuwaibia kwa kucharaza kila wanae muona mbele
lengo ni kulipiza kisasi kwa mwenzao kuuwawa
vituo vya polisi vimefungwa na polisi kukimbia
Quote By figganigga View Post
Hadi sasa maduka kibao yamefungwa. na biashara zimesimama. Waliondani wanatoka nje walio nje wanaingia ndani. Mimi sikufanikiwa kuwaona lakini nmepishana na watu wakikimbia.

Quote By fyddell View Post
Mi nipo knyama watu walikuw wnafunga maduka kw romours zilizokuwa zimeenea mitaani. Diffender mbili zimepita zikitokea mabatini kituo cha polisi na kupiga risasi moja hewani kabla hawajakunja kufuata akachube road ilielekeayo mwananyamala. Nothing has been known kuanzia nusu saa iliyopita.

Quote By Smart911 View Post
Yes, sinza wamepita. Tena wamepita nje ya nyumba yangu kabisa. Nimefunga milango na mageti yote nipo ndani tu na umeme umekatika. Ila kwa sasa pako shwari sijui wameeleka pande zipi. Ila ni hatari mtaa wote kimya kimya kabisa. Hata wenye za moto wanahofia endapo utaua mmoja
Breakingnews.......
Taarifa iliyotolewa na kituo kimoja cha redio cha EFM muda mfup uliopita,kumezuka kund moja maarufu km "PANYA ROAD" maeneo ya Ubungo na kufanya uhalifu wa mali na kuwaweka ktk hali ya waswas wakaz wa maeneo ya Ubungo! na taarif zilizopo sasa zinasema kundi hilo limefika maeneo ya Kinondon likielekea Msasan! tayar mamlaka zimepewa taarifa juu ya kund hilo ambalo linatumia visu,nondo na mapanga ktk kufanya uhalifu huo!
Kund hilo limeanza kufanya uhalifu huo jion saa 12 maeneo ya ubungo! kwa mujibu wa radio EFM,takriban maduka yote ya Ubungo yalifungwa jion kwa hofu ya kundi hilo!
sorce:EFM Radio
Like ·
wao wanarudi kwa kisasi.

0 comments:

Post a Comment