Kundi la
watu wanaodhaniwa ni Majambazi wakiwa na bunduki wameteka Kijiji cha Kimwani
katika wilaya ya Muleba Mkoani Kagera kisha kupora mali na kujeruhi watu kwa
risasi.
Habari
zimesema watu wakadhaa wamelazwa katika hospitali ya Rubya kwa matibabu baada
ya kujeruhiwa .
Mwandishi wa
harakatinews ameongea na mmoja wa maafisa wa afya katika hospitali ya Rubya na
kuelezwa kuwa waliopo katika hospitali hiyo hadi sasa ni watano baada yaw
engine 7 kuruhusiwa kutokana na kuwa na majeraha kidogo.
Kamanda wa
polisi mkoani Kagera Henery Mwaibambe hakupatikana mara moja baada ya simu yake
kuita bila kupokelewa ingawa habari ni kuwa ametuma timu ya makachero katika
eneo la tukio.
Tutaendelea kukujuza zaidi juu ya habari hizi
0 comments:
Post a Comment