Friday, January 23, 2015

unnamed (59)
Makamu wa Pili wa Rais wa Zanzibar, Balozi Seif Ally Idd akiwahutubia wageni mbalimbali waliohudhuria sherehe sherehe za miaka 50 ya CBE leo jijini Dar es salaam.
Chuo cha Biashara CBE kimetakiwa kufungua Tawi la chuo hicho Zanzibar na serikali itatoa ushirikiano kufanikisha ilikuweza kusogeza huduma ya chuo hicho na kuongeza wigo wa Udahili kwa wanafunzi wa Upande wa Zanzibar kwani kitawanufaisha wananchi hao bila ya kusahau utoaji wa elimu bora.
Kauli hiyo imetolewa na Makamu wa Pili wa Raisi wa serikali ya Mapinduzi Zanzibar Balozi Seif Ali Idd wakati wa maadhimisho ya miaka hamsini ya chuo hicho yaliofanyika jijini hapa huku akisema kuwa Mtu wa miaka hamsini si nongwa kuwa na watoto watano akiwa na maana ya wao ya chuo hicho kufungua tawi 5 Zanzibar.

Balozi Idd alisema kuwa Serikali ya SMZ itasaidia katika kuanzishwa kwa Tawi la chuo hicho Zanzibar ili kuongeza udahili wa wanafunzi wengi wenye weledi kwa upande wa Zanzibar kwenye sekta ya Biashara utakaosaidia ukuaji wa maendeleo endelevu na nyadhifa ndani ya serikali huku akiwataka kutoa elimu bora yenye viwango vya kitamaifa.

0 comments:

Post a Comment