Saturday, January 24, 2015

Displaying Dk hussein.JPG
NATIONAL BANK OF COMMERCE
BENKI YA TAIFA YA BIASHARA
TAARIFA KWA VYOMBO VYA HABARI
Dk Hussein ateuliwa kuwa mwenyekiti wa muda wa Bodi ya Wakurugenzi ya NBC
Dar es Salaam: Benki ya Taifa ya Biashara (NBC) imemteua Dk Kassim Hussein kuwa
mwenyekiti wa muda wa bodi ya wakurugenzi.
Hatua hiyo imetokana na kuteuliwa kwa aliyekuwa mwenyekiti wa bodi ya benki hiyo, Profesa
Mussa Assad, kuwa Mdhibiti na Mkaguzi Mkuu wa hesabu za Serikali (CAG) wa Jamhuri ya
Katika taarifa yake kwa vyombo vya habari iliyotolewa jijini Dar es Salaam leo, Mkurugenzi
Mtendaji wa Muda wa NBC, Bwana Pius Tibazarwa alisema Dk Hussein atashika wadhifa
wa
uenyekiti wa bodi ya benki hiyo mpaka pale atakapoteuliwa mwenyekiti wa kudumu wa bodi
Dk Hussein ni mhadhiri mwandamizi katika masomo ya kibenki na ya fedha katika Chuo cha
Usimamizi wa Fedha (Institute of Finance Management – IFM) cha Dar es Salaam. Dk Hussein
ni msomi mwenye Digrii ya Uzamivu katika masomo ya kibenki na Digrii ya Uzamili katika
masomo ya fedha. Aliteuliwa kuwa mjumbe wa bodi ya Wakaurugenzi wa NBC tangu mwaka
"Kwa mara nyingine tena, tunampongeza Profesa Assad kwa kuteuliwa kwake na kumtakia
kila la kheri katika kazi hiyo. Tunamshukuru pia kwa utumishi wake uliotukuka katika kipindi
chake kama mwenyekiti wa bodi ya Wakurugenzi ya NBC. NBC itaendelea kushirikiana nae
kuimarisha uwazi na uwajibikaji katika sekta ya fedha hapa nchini. Wakati huo huo, tunamtakia
kila la kheri Dk Hussein katika nafasi yake mpya ya uenyekiti wa bodi ya NBC," alisema
Profesa Assad aliteuliwa kuwa Mdhibiti na Mkaguzi Mkuu wa Hesabu za Serikali ya Jamhuri
ya Muungano ya Tanzania mnamo mwezi Novemba 2014 baada ya kuitumikia NBC kama
mwenyekiti wa bodi tangu mwaka 2006.VICTOR SIMON

0 comments:

Post a Comment