Saturday, January 24, 2015

Maandamano dhidi ya kupitishwa sheria mpya ya uchaguzi, katika mji wa Kinshasa, Januari 19 mwaka 2015.
Maandamano dhidi ya kupitishwa sheria mpya ya uchaguzi, katika mji wa Kinshasa, Januari 19 mwaka 2015
Na RFI
Hali ya machafuko imeendelea kwa siku ya tatu Jumatano Januari 21 katika mji mkuu wa Jamhuri ya Kidemokrasia ya Congo, Kinshasa.
Polisi iliingilia kati kwa kuwatawanya kwa mara nyingine tena vijana ambao wanaonekana kumpinga rais wa nchi hyio Joseph Kabila.
Jumatano alaasiri, hali ya utulivu ilirejea katika mitaa mbalimbali ya mji wa Kinshasa, lakini bado hali ya wasiwasi imeendelea kutanda katika maeneo mbalimbali ya mji huo, hususan katika mabweni ya chuo kikuu cha Kinshasa.

Baada ya masaa kadhaa ya utulivu Jumatano alaasiri, hali ya wasiwasi imeendelea kutanda katika chuo kikuu cha Kinshasa, baada tu ya kuondoka katika chuo hicho Waziri mkuu Matata Ponyo, ambae ni afisa wa kwanza wa serikali kutembelea chuo kikuu cha Kinshasa tangu kuanza kwa machafuko hayo Jumatatu Januari 19 mwaka 2015

0 comments:

Post a Comment