WAKATI diva wa filamu Bongo, Kajala Masanja ‘Kay’ akielezwa kuwa mambo yake hivi sasa yako kwenye mstari kwa kusajili kampuni yake ya mambo ya sinema, mwanamke aliyejitambulisha kwa jina moja la Pamela ameibuka na kumtaka muigizaji huyo kuacha kumfuata mume wake, data kamili hizi hapa.
Diva wa filamu Bongo, Kajala Masanja ‘Kay’.
Mwanamama huyo, anayefanya kazi ‘nzuri’ katika shirika moja kubwa nchini, aliliambia gazeti hili kuwa Kajala, amekuwa akitembea na mumewe aliyemtaja
kwa jina moja la Tanaluza ambaye kwa sasa yuko ndani katika gereza la Keko kwa kosa ambalo alikataa kulitaja.
“Jamani namtahadharisha Kajala, asije kunikuta pale, patakuwa hapatoshi, yeye si hodari wa kwenda kuangalia waume za watu, awe na haya, aende Ukonga akamuangalie mumewe, ushauri wa bure nampa,” alisema Pamela kwa jazba.
0 comments:
Post a Comment