Sunday, January 25, 2015

KATIKA pitapita zangu jana majira ya saa tisa alasiri walikumbana na nyani wa ajabu katika moja ya mitaa ya Tabata jijini Dar, nyani huyo aliyeonekana kuwa mchangamfu kama amemwagiwa ndimu alifanya mambo ya kustaajabisha uma kwani wengi walimshangaa wakati anaeletewa vifurushi vya takataka na wakazi wa mtaani hapo na kuvipakia mwenyewe kwenye mkokoteni kama binadamu huku akiwa na kibox kilichoandikwa (WEKA PESA HAPA TSH.200/=) hiyo ikiwa ni malipo ya uzoaji taka.

Huo hapo ndio muonekano wa box alilofungiwa kwenye mkokoteni kwa ili watu wawe wakitumbukiza pesa humo. Ama kweli dunia ina mambo yani mtu amekaa akafikiri, akaamua kubuni mbinu mbadala ya kujitafutia kipato kwa kumfuga nyani na kumpa mafunzo ya aina hiyo.

Picha kwa hisani ya masainyotambofu

0 comments:

Post a Comment