Posted by Williammalecela.com on Friday, January 23, 2015
 |
Je unakumbuka kisa cha wapenzi wawili waliozua gumzo nchini Kenya?
Msichana mhindi Sarika Patel kutoka familia tajiri na Timothy Khamala
mbukusu kutoka familia maskini kutoka Magharibi mwa Kenya kuoana? wakati
yao mapenzi yao yalijulikana kama Bukusu Darling, sifa kwa wanakoishi
wawili hao. Taarifa sasa ni kwamba mapenzi yao yamefika kikomo. Familia ya msichana Sarika ililaani sana mapenzi hayo kwani Timothy alikuwa anafanya kazi kwao kama mfanyakazi wa nyumbani. Na Sarika alipoamua kwenda kuishi na Timothy kama mume na mke familia yake ilimfukuza na kisha kumfuta kazi Timothy.
Wawili hao walioana kinyume na matakwa ya familia ya Sarika ambayo kwao
ilikuwa ni kama aibu kubwa sana kwa mtoto wao kutoka familia tajiri
kuolea na kijana asiyekuwa na mbele wala nyuma. Wakati taarifa ya
wawili hao ilipogonga vichwa vya habari nchini Kenya, Sarika na mume
wake walipata kazi katika kiwanda cha kutengeza Sukari kutoka kwa
wahisani. Lakini sasa kuna madai kwamba ndoa yao imevunjika baada ya
Sarika kulalamika kwamba Timothy amekuwa akimdhulumu na kumtusi kila
mara hali iliyosababisha wawili hao kutalakiana. Mtandao wa Standard
Digital umemnukuu Sarika akisema: "nilipokuwa mgonjwa , hakuwa hata na
muda wa kunipeleka hospitalini badala yake wazazi wake ndio
walionipeleka kutafuta matibabu. Mbali na hayo amekuwa akinichapa, ''
alisema Sarika huku akibubujikwa na machozi. Kwa sasa inaarifiwa anajuta sana kwa nini alikaidi amri ya wazazi wake.
''Ninajuta sana kwa nini sikuwasikiliza wazazi wangu na kuolewa kinyume
na mapenzi yao. Ninaomba radhi, natumai watanikubali kurejea nyumbani.
'' Sarika ambaye ni mtoto wa nne katika familia ya watoto watano,
ameamua kurejea nyumbani na kusema kamwe hatawahi kuwa na uhusiano wa
kimepenzi tena. Lakini wazazi wake wamempa masharti, mwanzo aishi na
rafiki yake huku akifanya uamuzi wa mwisho kuhusu anakotaka kuishi.
Anasema anahofia kwamba jamii ya wahindi haitamkubali tena kwani
hakuwasikiliza wakati walipomshauri kutoolewa na mwanamume mwafrika -BBC
Swahili.
|
0 comments:
Post a Comment