Monday, January 12, 2015

Katoto kachanga kalikotumbukizwa kwenye ndoo kwa zaidi ya saa 3.No! Manesi wa wodi ya wazazi katika Hospitali ya Rufaa ya Mkoa wa Morogoro wameingia kwenye kashfa nzito ya kusababisha kifo baada ya kudaiwa kumtumbukiza mtoto mchanga kwenye ndoo kwa zaidi ya saa 3. 

Tukio hilo ambalo kwa sasa ni gumzo mkoani hapa lilijiri hivi karibuni ambapo mwanamke aitwaye Zainabu lsmali, mkazi wa Kididimo jirani na Chuo Kikuu Cha Kilimo Cha Sokoine ‘SUA’ alishikwa na uchungu wa kujifungua na kukimbizwa katika hospitali hiyo kwa msaada wa jirani yake aliyejitambulisha kwa jina la Mama Sira Manga

0 comments:

Post a Comment