Sunday, January 11, 2015

Mshenga anayefahamika kwa jina moja la Isaya akipeleka posa kwa akina Lulu Elizabeth Michael.
STAA ndani ya Tasnia ya Filamu Bongo, Elizabeth Michael ‘Lulu’, amepelekewa barua ya uchumba kutoka kwa mfanyabiashara mmoja jijini Dar na kumfanya mama mzazi wa Lulu, Lucresia Karugila abaki ameshangaa.Tukio hilo lilitendeka Januari 8, mwaka huu, Mbezi Beach jijini Dar es Salaam ambako ndiko yaliko makazi ya Lulu na mama yake huyo.MSHENGA NI MPAMBE

Kwa mujibu wa watonyaji wetu ambao waliwataarifu mapaparazi wetu wa Kitengo cha Kufichua Maovu (OFM) kuhusu barua hiyo na kutia timu nyumbani hapo, mtu aliyepewa kuifikisha kwenye familia hiyo ni mpambe mkubwa wa mfanyabiashara huyo aliyetajwa kwa jina moja la Isaya, mkazi wa Kinondoni B, Dar es Salaam ambaye sasa amekuwa mshenga pia.
Staa ndani ya Tasnia ya Filamu Bongo, Elizabeth Michael ‘Lulu’.MSHENGA GETINI KWA AKINA LULU

0 comments:

Post a Comment