Balozi Seif alifahamisha kuwa Matamasha ya Biashara hutoa fursa ya kukuza Sekta ya Utalii kwa kuhudhuriwa na wageni mbali mbali kutoka nje.
Alisema nchi nyingi Duniani zinafaidika na Matamasha makubwa ya kibiashara kama vile Tamasha la Dubai Shoping Festival linalokusanya zaidi ya Wageni Milioni 4.4 na kuchangia pato la Taifa zaidi ya Bilioni 15.
Alieleza kuwa Serikali itaendelea kushirikiana na Wafanya Biashara wa Zanziba,r Tanzania na Afrika Mashariki katika kuhakikisha sekta ya Biashara inazidi kukua na kuimarika ili kuongeza pato la Taifa .
Sambamba na hayo alisema Serikli itaendelea kushughulikia changamoto zinazoikabili Sekta ya Biashara kama vile upatikanaji wa vifungashio, kuanzisha mfumo wa nambari za utambulisho wa bidhaa (barcodes) na kufikia Viwango vya Biashara Kimataifa.
“Ni vyema Matamasha ya aina hii yakajumuisha maonyesho ya Utamaduni wa Mzanzibari zikiwemo kazi za Sanaa, Vyakula vya asili na Muziki wa mwambao ambao unaendelea kutoweka” Alisema Makamu wa Pili.
Ameitaka Wizara ya Biashara, Viwanda na Masoko kulitangaza zaidi Tamasha la Biashara na kuanzisha eneo maalum la maonyesho ya Biashara hapa Zanzibar.
Balozi Seif alitoa shukurani zake kwa Taasisi za Serikali na watu binafsi, Makampuni, Wafanya Biashara wa ndani na nje ya nchi kwa kushiriki Tamasha hilo.
Nae Waziri wa Biashara Viwanda na Masoko Nassor Ahmed Mazurui alisema zaidi ya Wafanya Biashara 160 watashiriki Tamasha la mwaka huu.
Alisema Tamasha hilo linalengo la kuitangaza Zanzibar Kiutalii na Kibiashara kwa kuandaa mazingira mazuri ili kuleta kivutio kikubwa kwa washiriki na wanunuzi.
0 comments:
Post a Comment