Na Laurent Samatta MSANII wa kitambo kwenye tasnia ya filamu Bongo, Yvonne Cherly ‘Monalisa’ (33) amesema kuwa yeye siyo gubegube kwani alishawahi kukaa ndani ya ndoa lakini sasa ameamua kutulia.
“Mimi si gubegube, nikiamua kurudi na kufunga ndoa naweza tena nitaolewa kama Yvonne Cherly kwani ndilo jina langu halisi. Ninachokiwaza kwa sasa si kukaa ndani ya ndoa bali namna kazi zangu zitakavyoweza kuonekana zaidi,” alisema Monalisa.
0 comments:
Post a Comment