Tuesday, January 20, 2015

Mwanamke (Doreen John Mlemba) anayedaiwa kukamatwa na unga.
MWANAMKE mmoja aliyetambuliwa kwa jina la Doreen John Mlemba, mwenyeji wa Same mkoani Kilimanjaro, mwishoni mwa mwaka uliopita alikamatwa kwa kuhusishwa na shehena ya madawa ya kulevya aina ya Heroin, yenye thamani ya shilingi bilioni 2.5.
Madawa hayo yalikutwa kwenye nyumba moja iliyopo eneo la Ununio, Tegeta jijini Dar es Salaam, ambayo ni mali ya Mbunge wa CCM (Jina linahifadhiwa) wa jimbo moja la mikoa ya Kanda ya Ziwa, Uwazi limefukunyua.
Taarifa toka vyanzo mbalimbali makini, zinasema majirani wa nyumba hiyo walikuwa na mashaka na kinachofanyika ndani ya nyumba hiyo, kwani licha ya ukubwa na kukamilika kwa ujenzi wake, lakini haikuwa ikikaliwa na mtu na mara chache, watu walionekana wakiingia na kutoka bila kujulikana walichokuwa wakikifanya.
Kutokana na hali hiyo ya wasiwasi, wasamaria wema walitoa taarifa kwa Jeshi la Polisi ambalo liliifanyia kazi habari hiyo na kufika kwenye nyumba hiyo na kujaribu kugonga lakini bila mafanikio yoyote.
“Baada ya kugonga, ndipo polisi hao walipoamua kuvunja mlango na kufanya upekuzi katika sehemu zote ndani ya nyumba hiyo, ambapo walifanikiwa kulikuta sanduku ambalo baada ya kufunguliwa, zikagundulika kilo 35 za madawa ya kulevya aina ya Heroin,” kilisema chanzo chetu kilichoshuhudia zoezi hilo.

0 comments:

Post a Comment