Mara baada ya kumnasa na kumlamba picha akiwa na wenzake ambao nao kama yeye walikuwa wamevaa nguo fupi yaani nusu utupu, alianza kuangua kilio hasa alipokuwa akihojiwa kwa nini anajihusisha na biashara hiyo hatarishi katika maisha yake.
“Jamani mmenipiga picha mtanipotezea kazi yangu, jamani mimi nimeajiriwa, ni mfanyakazi wa ndani kwa mheshimiwa Mikocheni (Dar), nafanya kazi za ndani hii yote ni kujitafutia riziki nje ya kazi,” alilalama binti huyo aliyekadiriwa kuwa na umri kati ya miaka 20 hadi 23.
“Mshahara wangu ni mdogo sana, nalipwa shilingi elfu 50 kwa mwezi, nina watoto wawili kijijini hivyo hautoshi. Kama vipi nitafutieni kazi nitaacha kuuza mwili,” alisema.
Alipoulizwa namna anavyotoka kwa bosi wake kwenda kujiuza, hausigeli huyo alisema kwamba huwa anakula dili na walinzi wa bosi wake usiku wakiwa wamelala anatoka na akirudi freshi anawakatia walinzi chao.
Aliendelea kueleza kwamba kuna siku nyingine huwa anarudi nyumbani akiwa amevuna fedha nyingi kuliko mshahara wake.
“Hii kazi yangu inaniingizia kipato kikubwa sana kuliko mshahara,” alisema hausigeli huyo
0 comments:
Post a Comment