Mbunge wa Jimbo la Chalinze, Ridhiwani Kikwete akikagua vyumba vya madarasa vya Shule ya Msingi Kibindu, wilayani Bagamoyo, Pwani vilivyobmoka na kuezuliwa paa kutokana na mvua kubwa iliyonyesha hivi karibuni. Ridhiwani yupo katika ziara ya kikazi ya kutembelea vijiji 40 jimboni humo.Pia Ridhiwani alishauri shule hiyo yenye majengo yaliyojengwa tangu 1952 ifungwe ili kuepusha maafa zaidi hadi itakapojengwa upya.
Ridhiwani akimtwisha ndoo ya maji mmoja wa akina mama wa Kijiji cha Kwa Msanja wakati wa uzinduzi wa Kisima cha Maji kilichojengwa kwa fedha za mfuko wa jimbo kwa gharama ya sh. mil. 13.
Ridhiwani akinunua ndizi na kuzigawa kwa watoto katika Kijiji cha Kwa Msanja wakati wa ziara yake jimboni Chalinze jana.
Ridhiwani akihutubia mkutano wa hadhara katika Kijiji cha Kwa Mduma, Kata ya Kibindu, ambapo aliwahidi kuboresha barabara na mawasiliano ya simu
VICTOR SIMON
0 comments:
Post a Comment