Na Waandishi Wetu
HALI
inazidi kuwa mbaya kwa mastaa wawili wa muziki wa Bongo Fleva
wanaogombea unyota kimuziki, Nasibu Abdul ‘Diamond Platnumz’ na Ali
Saleh Kiba, safari hii yameibuka mapya kwa kila msanii kuogopa kumshika
mkono mwenzake kutokana na imani za kishirikina.
Mashabiki wa Mbongofleva Ali kiba waliionyesha kumkubali zaidi kuliko, 'Daimond Platnumz' katika viwanja vya Leaders Club.
TUJIUNGE LEADERS
Matukio
hayo ya kusisimua yaliwatia hofu kubwa mashabiki na wadau wa muziki
Bongo muda mfupi kabla ya nyota hao kukaribishwa stejini kwenye Viwanja
vya Leaders Club, Kinondoni jijini Dar, mwishoni mwa wiki iliyopita.
HIRIZI ZAKUTWA UWANJANI
Kwa
mujibu wa wanahabari wetu, katika Viwanja vya Leaders, Kinondoni,
kulikutwa hirizi zilizozagaa, zilizodaiwa kudondoshwa na vijana
waliokamatwa wakiwa wamevalia sare zenye majina ya mastaa hao wawili.
Moja ya Hirizi iliyotupwa katika viwanja hivyo.
Katika
hali ya kushangaza, mmoja wa mashabiki waliohudhuria onyesho hilo
ambaye aliziona hirizi hizo, aliwashangaza mashabiki wenzake alipodai
kuwa anaiona mojawapo ikitweta mithili ya inayopumua!
“Oneni
wadau, hii hirizi si inapumua, iangalieni vizuri,” alisikika shabiki
huyo na kuwaacha watu wakiwa wamepigwa na butwaa kuona vitendo hivyo vya
kishirikina katika eneo la burudani.
Wakati
matukio hayo ya kukutwa kwa hirizi hizo yakiendelea, Diamond, baada ya
kupanda jukwaani kabla ya kuanza kuimba, akajikuta akiteleza na kuanguka
jukwaani na kusimama mwenyewe huku vijana wanaodaiwa kuwa ni wa Timu
Kiba wakipiga kelele kwa nguvu kuashiria kuwa walipendezewa na kitendo
hicho kutokea.
Mashabiki waliotinga katika shoo hiyo wakishuhudia hirizi zilizo zagaa katika viwanja hivyo vya Leaders.
Pamoja
na Diamond kula mwereka hadi chini, hali ilizidi kuwa mbaya kwake baada
ya muziki kuanza kusikika vibaya huku ukiwa unakatakata, kitendo
kilichoamsha hisia kuwa kulikuwa na ushirikina unaoendelea ili kumshusha
kisanii kwa kuonekana amefanya vibaya katika shoo hiyo.
CHUPA ZARUSHWA
Baada
ya kuona hali inazidi kuwa mbaya huku chupa za maji zikirushwa jukwaani
hapo na baadhi zikimpiga na nyingine akizikwepa wakati akiendelea
kupiga shoo, Diamond aliamua kutumia akili ili kuzima kelele hizo kwa
kuanza kumwaga noti.
Kikosi cha ulinzi kikiwajibika kudhibiti vijana walioonyesha tabia korofi.
Ishu
hiyo iliwafanya mashabiki na Timu Kiba kuachana na zoezi hilo na kuanza
kusukumana kugombea noti hizo za elfu mbilimbili ambapo alimwaga kwa
awamu tatu.
SADAKA?
Wakati
akizidi kuwatupia noti mashabiki, Diamond alisikika akisema kuwa pesa
hizo ni maalum kwa mashabiki kwani ni sadaka kwao kutokana na sapoti
kubwa wanayompa ingawa hataweza kumpa kila mmoja.
Makamanda wa Polisi na kikosi cha Ulinzi wakihakikisha usalama unakuwepo kwa mastaa waliopangwa kutoa shoo.
DIAMOND KAMA MICHAEL JACKSON
Hata hivyo, baadhi ya mashabiki waliokuwa wakisukumana na kuokota noti hizo walisikika wakisema:
“Huu mchezo alikuwa akiufanya Michael Jackson (Mwanamuziki marehemu wa Marekani) tena alikuwa akitumia ushirikina na Freemasons.
“Michael
alikuwa anadaiwa kumwaga fedha hizo zilizokuwa na nguvu ili kuwafanya
wale waliokuwa wakimzomea kukaa kimya,” alisikika shabiki mmoja akisema.
MSHANGAO
Katika
hali ya kushangaza zaidi, Diamond alivua tisheti na vesti ya ndani na
kujifuta jasho kisha kuwarushia mashabiki huku akijua wazi kuwa amefutia
jasho lililokuwa likimiminika mwilini mwake kama maji.
.jpg?width=650)
Mbongofleva, Nasibu Abdul ‘Diamond Platnumz’
KIBA HAKUTAKIWA KUZUNGUMZA?
Wakati
matukio ya kushangaza aliyokuwa akiyafanya Diamond na yale ya kurushiwa
chupa za maji machafu na yenye mikojo yakiendelea, ilidaiwa kuwa Kiba
alipoingia kwenye chumba cha wasanii hakutaka kuzungumza na mtu yeyote
huku ikidaiwa kuwa hiyo ni ishara kubwa kuwa hakutakiwa kuzungumza na
mtu kwani angeweza kupoteza nguvu za kufanya shoo.
POLISI MZIGONI
Wakati
mashabiki wakizidi kuwa na wasiwasi juu ya wasanii hao, jeshi la polisi
lililokuwa na zana zote za kukamatia wahalifu, walianza doria ya
kukamata vijana ambao wanadaiwa kuwa ni Timu Kiba waliokuwa wakibishana
na kutupa chupa zenye mikojo na maji huku wakipokea kipigo kama cha
mbwa mwizi.
Mbongofleva, Ali Saleh Kiba.
KIBA ARUKA UKUTA
Awali
kabla ya shoo hizo kuanza matukio ya kishirikina yalijidhihirisha zaidi
baada ya Ali Kiba kuingia uwanjani hapo kwa njia ya kuruka ukuta na
hata alipozama kwenye chumba maalum walichokuwa wametengewa wasanii
hakuweza kushikana mikono na wenzake.Wasanii ambao Ali Kiba aliwachunia
ni AY, MwanaFA, Shaa, Shilole, Vanessa Mdee na Jux, ambao wote aliwakuta
ndani ya chumba hicho.
Imeandaliwa na Gladness Mallya, Musa Mateja, Chande Abdallah, Mayasa Mariwata, Shani Ramadhani, Denis Mtima na Laurent Samatta
0 comments:
Post a Comment