KABANG! Picha za staa wa sinema na Bongo Fleva, Zuwena Mohamed ‘Shilole Kiuno’ zinazomuonesha live akiwa chumbani tena kitandani kimahaba na mwandani wake, Nuh Mziwanda zimevuja, Risasi Jumammosi linazo kwenye makabrasha yake.
NYOTA wa Nyimbo za Injili Bongo, Rose Mhando (pichani)amefungukia eneo fupi la maisha yake magumu ambapo alisema amewahi kutekwa kwa bastola na mwanaume mmoja, akampeleka msituni ambako alimlazimisha kuwa naye kimapenzi lakini akadunda.
Siku chache baada ya kumwagwa na Wema Isaac Sepetu ‘Beautful Onyinye’, Mbongo Fleva, Nasibu Abdul ‘Diamond Platnumz’ amenaswa kwenye mahaba mazito na msanii, mtangazaji, mjasiriamali, tajiri na mrembo mkali kuliko wote Afrika Mashariki, Zarinah Hassan a.k.a Zari au Boss Lady.
Ni sheeedah! Msanii wa Bongo Fleva, Nasibu Abdul ‘Diamond’ amecharukia gari aina ya BMW 545 alilozawadiwa mwandani wake, Beautiful Onyinye wa Bongo, Wema Isaac Sepetu ‘Madam’ ambaye ni Miss Tanzania 2006/07, akipinga gari hilo kupewa na meneja wake, Martin Kadinda.
MISS Tanzania 2006/07 ambaye ni staa wa sinema za Kibongo, Wema Isaac Sepetu ‘Beautiful Onyinye’, amevunja ukimya kwa kuamua kuanika kisa cha yeye kummwaga aliyekuwa mwandani wake, nyota wa Bongo Fleva, Nasibu Abdul ‘Diamond Platnumz’.
BAADA ya kula bata za kutosha Bongo, wakati wakisindikizana kimahaba, staa wa Bongo Fleva, Nasibu Abdul ‘Diamond Platnumz’ na mrembo mkali kutoka Uganda, Zarinah Hassan a.k.a Zari au The Boss Lady, wamezua gumzo kwenye Uwanja wa Ndege wa Kimataifa wa Julius Nyerere jijini Dar, Ijumaa lina mchapo kamili.
KIFO cha tajiri maarufu mjini Bukoba, Leonard Mtensa (50) ambacho kimetingisha kanda nzima ya ziwa, kilichotokea dakika chache baada ya marehemu kudaiwa kufanya mapenzi ndani ya gari lake, sasa mambo hadharani juu ya kila kitu kilichotokea, Risasi Jumamosi linakupa mkanda mzima.
DUNIA hii basi tena! Ni tukio la kusisimua ukilisoma mwanzo hadi mwisho lakini ni la kikatili sana! Ni lile la ndugu wawili warembo, dada na mdogo wake kukutwa wamekufa kwa kunyongwa ndani ya nyumba aliyokuwa amepanga mmoja wao huku muuaji akidaiwa alivaa taulo lenye weupe wa kufifia akitokomea zake.
KWA mara ya kwanza ndani ya Global TV Online ya Global Publishers, supastaa ndani na nje ya Bongo kutoka muziki wa Kizazi Kipya, Nasibu Abdul ‘Diamond Platnumz’ amewafungukia waliowahi kuwa wapenzi wake, Jokate Mwegelo ‘Kidoti’, Wema Sepetu ‘Madam’ na Penniel Mungilwa ‘Penny’ kuwa waligoma kumzalia mtoto.
0 comments:
Post a Comment