![]() |
Fleva , Nasibu Abdul ‘ Diamond Platnumz’ alilompa
aliyekuwa mwandani wake , Beautiful Onyinye , Wema
Isaac Sepetu ‘ Madam’ limezua mapya ambapo baada
ya kudai linamchefua sasa anadaiwa kuwa analiuza
kwa kigezo kwamba hataki gundu mwaka huu mpya wa
2015.
Gari jipya aina ya Nissan Murano la staa wa Bongo
Fleva , Nasibu Abdul ‘ Diamond Platnumz’ alilompa
aliyekuwa mwandani wake , Beautiful Onyinye , Wema
Isaac Sepetu ‘ Madam ’
KUMBE LIPO KWA DALALI
Habari za kiwango kutoka kwa mnyetishaji wetu zilidai
kwamba gari hilo lipo kwa dalali wa kike maarufu
ajulikanaye kwa jina moja la Tindwa kwa ajili ya
kulitafutia mteja.
NI KISASI ?
Ilidaiwa kwamba , Wema ameamua kufanya hivyo kwa
kuwa ana kisasi na hasira kwa Diamond kwa kuwa
jamaa huyo kwa sasa anadaiwa kutoka kimapenzi na
staa wa Uganda , Zarinah Hassani ‘ Zari au The Boss
Lady ’ .
“Watu wanadhani Wema anafurahishwa na Diamond
kutupia mapicha na Zari baada ya kuwasifia juzikati .
“Ukweli ni kwamba hivi sasa Wema anakereka sana na
jinsi Diamond anavyoweka mapicha yake na Zari
wakiwa sehemu mbalimbali na anaona kuwa na gari
ambalo amepewa zawadi na Diamond ni kujipa kero
zisizokuwa na sababu hivyo ameamua kuliuza , ”
kilisema chanzo hicho .
Aliyekuwa mwandani wa Nasibu Abdul ‘ Diamond
Platnumz’ Wema Isaac Sepetu ‘ Madam ’ .
HALIJAPATA MTEJA
Mpashaji wetu huyo alizidi kunyetisha kwamba pamoja
na gari hilo kuwa sasa bado liko sokoni lakini
halijapatia mteja wa kulinunua kitu ambacho kinazidi
kumkera Madam.
“Bado gari halijapata mteja ‘ so’ kitendo hicho
kinamkera sana Wema kutokana na gari hilo kutouzika
mapema kwa maana kila anapoliona hajisikii vizuri
kabisa, ” kilisema chanzo hicho kwa sharti la kutotajwa
gazeti kwani ni ‘ besti ’ mkubwa wa Wema.
WEMA ANASEMAJE ?
Baada ya kupewa ubuyu huo, gazeti hili lilimsaka Wema
ambaye alipopatikana alidai yupo bize akiandaa shoo
zake za mkoani Dodoma na Morogoro.
“Ngojeni kwanza nimalize shoo zangu za mikoani. Kwa
sasa nipo Dodoma nikimaliza naenda Morogoro, ”
alisema Wema kwa ahadi kuwa atafafanua suala hilo
vizuri akitulia.

0 comments:
Post a Comment