Posted by Williammalecela.com on Friday, January 16, 2015
 |
| Hizi picha mbili niliipiga na wafanyakazi wa ICL miezi 2 iliyopita nilipoenda kufanya makubaliano na nao kuhusu kuitangaza Cocacola n i kuweka record straigh tu!! |
 |
Wiki hii imekuwa na ishu moja nzito sana kuhusu kitendo cha kampuni ya Cocacola kutengeneza makopo yenye majina ya Wasanii na watu mbali mbali wenye majina maarufu na hata wasiokuwa isipokuwa tu kwamba Cocacola kupitia ICL waliamua nani wanaowaamini kuwa na ushawishi mkubwa kwenye jamii wawe wa kwanza kupewa makopo hayo. Kwa bahati nzuri binafsi nilikuwa mmoja waliobahatika kuchaguliwa na Cocacola as watu wa kwanza wa kupokea makopo hayo something I am very grateful to the Company kwa sababu so since Monday nilipopata kopo hilo na kulitangaza tayari nimeweza kusaini mikataba miwili mipya na kampuni mpya ya Kimarekani nchini ambayo 100% uamuzi wao wa kunipa mkataba wa kuwatangaza umetokana na kuwa impressed na mimi kuwa na kopo la kampuni yenye chanzo chake Marekani, nimesaaini nao mkataba huo Jumatano wiki hii na jana nimesaini mkataba mpya wa kuitangaza kampuni ya One Extreme Solutions TZ na again ni kutokana na kopo hilo hilo la Cocacola ndio maana ninasema Cocacola nawapa SHIKAMOO for the best gift ever in my life. Now kuna Mwanasheria mmoja ambaye simfahamu wala sijawahi kukutana naye wala kumuona uso kwa uso akaamua kuanza kurusha maneno mazito sana akituponda wote tuliopokea haya makopo kwamba tumeibiwa na Cocacola ambao kwa maneno yake amewaita ni "Wanyonyaji", binafsi nikaaamua kuweka record straight kwamba sio kweli Cocacola haina makosa yoyote haikutumia bunduki kumpa mtu yoyote kopo, na kwamba tulipokea hayo makopo tumeibiwa kwa sababu binafsi nilishaingia makubaliano ya kusaidia matangazo yao Miezi Miwili iliyopita hata kabla wazo la kutengeneza haya makopo halijabuniwa na hata walipolibuni walinifahamisha mapema sana mwezi uliopita kati kati kwamba watanitengenezea kopo lenye jina langu which to me was just a part of the deal I had tayari with them Mwezi mmoja na nusu kabla, na sikuwa na tatizo kwa sababu tayari nilishaingia makubaliano nao, isipokuwa niliwafahamisha wazi kwamba kama watayauza makopo hayo madukani basi tutakuwa na mkataba tofauti lakini kopo moja lenye jina langu sikuwa na tatizo infact nilifurahia sana the idea kwa sababu mimi ni mbepari by my blood so nilijua nikilipata tu nitalitumia sana kwa faida yangu ndio maana hata nikaweza kuvuta mikataba hii miwili wiki hii. Lakini to my shock Mwanasheria yule akaamua kuanza kunirushia maneno mengi mazito sana mpaka kuanza kutabiri kuhusu umri wangu kama vile ananijua au ni mganga wa Kienyeji, akaenda mbali sana mpaka kudai kwamba mimi ninaishi kwenye Gorofa la NHC ambalo ni nyumba ya Baba yangu, that was a big shock maana toka nimezaliwa sijawahi kusikia kuna baba wa mtu hapa Tanzania anamiliki gorofa hata moja la NHC so I was like huyu jamaa ni Mwanasheria wa nini hasa? Kwenye maneno yake akadai nina miaka 56 kwa hiyo ni umri wa baba yake na kwamba nimechoka kiakili, sasa again nikashangaa zaidi maana huo sio umri wangu na wala sijafikia huko na besides alichonishangaza zaidi ni kudai kwamba miaka 56 mtu unakuwa kama baba yake sasa akiwa na maana kwamba baba yake hana akili kwa vile ana miaka 56 that was a shock to me kwamba Tanzania kuna Mwanasheria anaweza kuandika maneno ya hovyo kama hayo so nikamjibu tena kwenye my Instagram Wall. Lakini jana usiku kwa vile simfahamu huyu Mwanasheria nikaamua kuwauliza wanomjua kwa karibu sana wakaniambia hata wao hawataki kumsikia kwa sababu hivi siku za karibuni amepata pesa kidogo so amekuwa na jeuri sana na hawa ni Wanasheria wanaofahamika hapa mjini na pia Wana pesa kwa muda mrefu sana hapa mjini so nikaamua kuachana na Mwanasheria. Leo nimeamshwa na simu za watu wengi wakiniambia kuhusu ishu hii tena kuwa kwenye blog moja ambayo mimi huwa siipitii kabisa kwa sababu ya kukosa muda so nikaamua kupitia mwenyewe na kusoma maneno mengi ya kitoto kuhusu kuishambulia kampuni ya Cocacola na wale wote tuliopokea hayo makopo nafikiri hili la makopo nimelijibu tayari isipokuwa sasa nataka kujibu hoja ya blog hiyo kuhusu matangazo ya biashara ndani ya blogs, Ninasema hivi mimi binafsi nimeifungua blog hii mwaka 2012 since then nimefanya matangazo na makampuni mengi sana na mpaka leo nikutokana na matangazo hayo ndio maana hii blog sasa ni kampuni iliyosajiliwa Brela na ninailipia kodi Serikalini na ni Kampuni inayojitegemea na kuajiri Vijana kama 3 na sasa hivi ninategemea kuhamisha ofisi zake toka ofisi ndogo tuliyokuwa huko Gerezani na kuhamia Posta mpya mjini kabisa next week na kwenye ofisi kubwa zaidi katika gorofa ya pili ya Jengo la Tancot House. Ninapoandika sasa hivi blog hii ina mikataba ya matangazo ya Makampuni kama Vodacom, Airtel, Windhoek Beer, NSSF, PSPF, na mengineyo ambayo ni malipo yao ndio yameifanya blog hii kusimama kama Kampuni, sasa tunaposikia maneno ya kijinga kama niliyoyaona huko tunashangaaa kwamba kwani kuna tatizo gani jamani maana haiwezekani tatizo likawa kopo tu la Cocacola lazima kuna zaidi maana maneno yamekuwa mengi sana na kelele nyingi sana as if hawa wanaolia lia wanatulisha au wanatulipia maisha hapa mjini kumbe wala hatujawahi kuwaomba anything wote tupo mjini tunahangaika na maisha na kila mtu anakula kwa urefu wa kamba yake sasa tatizo lipo wapi? Nawaomba wale wote mnaolia lia na haya makopo please tumieni busara kidogo tu ya kujua kwamba sio nyinyi tu wenye akili kama mnavyodai hapana na si kweli kwamba mnaijua sana Sheria kuliko sisi wengine wote, hapana ila ninahisi mna tatizo kubwa kuliko mnalolisema lisemeni tu kuliko kuzunguka mbuyu. Again thanks sana Cocacola kwa kunitengenezea hili kopo maana hata Mjukuuu wangu atalikuta na nitaendelea kulitumia as a bargaining tool kwenye meza za mikataba ya kutangaza biashara ya makampuni!! MUNGU AIBARIKI TANZANIA KWAMBA LEO SOME OF US CAN MAKE MONEY JUST KWA KUSUBIRI MATANGAZO YA BISHARA TU!! - Le Mutuz
|
0 comments:
Post a Comment