Na Andrew Chale
USIKU wa Old is Gold taarab unatarajiwa kurindima ndani ya ukumbi wa Safari Carnival, Mikochezni B, kwa wadau kupata burudani ya muziki wa mwambao wa kizamani.
Kwa mujibu wa waandaji wa usiku huo, Mkurugenzi wa Fabak Fashions, Asia Idarous Khamsin alieleza kuwa ni kila Jumapili ndani ya ukumbi huo utakuwa na burudani ya kipekee kwa nyimbo za mwambao pamoja na ‘surprise’ mbalimbali kwa watakaofika hapo.
“Kila jumapili kwa kiingilio cha sh 5,000 tu. Wapenzi wa muziki wa mwambao watashuhudia shoo ya Usiku wa Old is Gold ndani ya Safari Carnival” Alisema Asia Idarous
Aliongeza kuwa, mbali na burudani ya taarab za zamani pia kutakuwa na ‘Surprise’ mbalimbali” kwa wadau watakaojitokeza kwenye usiku huo.
Aidha, Asia Idarous alisema usiku huo, pia umedhaminiwa na Safari Carnival, Fabak fashions, Clouds
fm, Gone Media, Maji Poa, Michuzi Media Group na wengineo.
0 comments:
Post a Comment