Posted by Williammalecela.com on Tuesday, January 13, 2015
 |
Siku ya tarehe 11.01.02 wadau wa "Social Media Network Citizens", ambao
ni watumiaji wa mtandao wa kijamii wa Twitter walifanya awamu ya pili
ya zoezi la kukabidhi madawati 241 kwa shule ya msingi ya Mjimwema
iliyopo kwenye kata ya Mjimwema, Jimbo la Kigamboni.
Katika awamu ya kwanza, wadau hawa walikabidhi madawati 45. Jumla ya Tsh
30.5 millioni zimechangwa na wadau hawa na zimetumika kutengeneza
madawati 286 yaliyotolewa hadi hivi sasa.
Mchango huu wa madawati umewezesha kutatua tatizo la madawati kwenye
shule hii kwa asilimia 80% na kuwezesha wanafunzi 858 ambao ni asilimia
75% ya wanafunzi wote kukaa kwenye dawati.
Mgeni Rasmi kwenye makabidhiano haya alikuwa Mbunge wa Jimbo la Kigamboni, Dkt Faustine Ndugulile.
Pichani: Mbunge wa Kigamboni (kulia) akikabidhi MOJA ya dawati kwa
Mwalimu Mkuu (Kushoto) huku wakishuhudia na Bw Irinei Kiria (Mbunifu wa
harambee hii), Bi Germana Ibreck (Mtunza fedha), Dkt Mwele Malecela na
Afisa Elimu toka Manispaa ya Temeke.
Mtunza fedha wa Social Media Network Citizens Bi Germana Ibreck akiwa na wanafunzi wa shule ya Mjimwema.
Mgeni Rasmi, Mbunge wa Kigamboni, akiwa katika picha ya pamoja na wadau wa Social Media Network Citizens na walimu.
Mwisho, shule hii bado inahitaji madawati 70 ili watoto wote waweze kuwa
na dawati. Vile vile Ofisi za walimu zina upungufu wa samani. Wadau
wameanza raundi ya tatu ya michango kwa ajili ya kumaliza tatizo la
madawati kwenye shule hii.
Wadau wanaotaka kuchangia wanakaribishwa kuwasiliana na waratibu (@AnnieTanzania na @IrineiKiria) kupitia mtandao wa Twitter. |


0 comments:
Post a Comment