Monday, February 2, 2015

Ethiopia Mugabe AU
 Mwenyekiti Mpya wa Umoja Wa Afrika(African Union) amesema Africa itajiondoa International Criminal Court (ICC). Amesema hiyo itakua agenda katika mkutano wa umoja huo utakaofanyika mwezi wa sita mwaka huu nchini Afrika Kusini. Rais Mugabe(Zimbabwe), ameyasema hayo  tarehe 31 Januari, 2015 wakati wa kufunga mkutano wa 24 wa umoja huo Addis Ababa nchini Ethiopia.
Ametoa wito kwa Africa kuunda "The African Court of Justice and Human Right" itakayoshughulikia kesi za Afrika ambazo zinafanana na zile za ICC. 

Akiunga mkono hoja hiyo, Raisi wa kenya, Uhuru Kenyatta ameahidi kutoa $ 1M kwa ajili ya uanzishwaji wa "The African Court of Justice and Human Right".

1 comment:

  1. Kwa kuanzisha mahakama ya haki za binadamu ya Africa nimewakubali kuwa mko juu sasa, pia ni fundisho kwa hiyo mahakama ya the Hague ambayo ina uoga kwa mataifa makubwa ila inajua kazi linapokuja suala la Africa tu, mpaka leo wameshindwa kuwatia hatiani kina Netanyau au George Bush kwa mauaji ya kutisha ya halaiki huoni walikuwa ni wanafiki tu?
    Big Up viongozi wa Africa kwa kuunda mahakama ya Africa.

    ReplyDelete